Katibu wa chama cha waandishi wa habari za michezo na burudani
mkoa wa Arusha,(TASWA- Arusha) Mussa Juma
Na Woinde
Shizza,Arusha
Mkuu wa
mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda,anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika
tamasha la 10 la vyombo vya habari vya mkoa wa Arusha. ambalo
litafanyika Agosti 29 katika uwanja wa sheikh Amri Abeid.
Akizungumza
na waandishi wa habari Palace hoteli jana mwenyekiti wa TASWA mkoa wa
Arusha, Jamila Omar na Katibu wa TASWA Arusha, Mussa Juma walisema
maandalizi yote muhimu yamekamilika ikiwepo ujio wa timu ya TASWA kutoka
jijini Dar es Salaam.
Omar alisema Kauli
mbiu ya Mwaka huu ya Tamasha hilo ni
kuwa,Uchaguzi bila vurugu inawezekana na timu zitachuana katika
michezo ya Soka, mbio zamagunia, kuvuta kamba, kukimbiza kuku na mpira
wa pete.
Alisema
mdhamini Mkuu wa Tamasha hilo ni Kampuni ya Bia nchini(TBL), ambapo
wadhamini wengine ni TANAPA, Faidika, Mega Trade Investment,na SBC(T)
Ltd.
Omar aliwataja
wadhamini wengine kuwa ni, Shilika na nyumba nchini(NHC), Kampuni ya
Tanzanite One,Coca cola na Big Expedition.
Akizungumzia
tamasha hilo, Afisa matukio ya TBL Arusha, Chris Sarakana aliwataka
wanahabari na wakazi wa mkoa wa Arusha kujitokeza na kuahidi TBL
itaendelea kushirikiana na wanahabari.
Awali
Katibu wa TASWA mkoa wa Arusha,Mussa Juma alitaja timu nyingine
zitakazoshiriki ni TASWA Arusha, AJTC. Habari Maalum,Radio 5, Radio
,Faidika,Mj radio, Arusha one na ORS kutoka mkoa wa Manyara.
Alisema
kabla ya Tamasha wanahabari watatembelea
hifadhi ya Taifa ya Arusha
vile vile kiwanda cha Bia nchini(TBL) mkoa wa Arusha na viwanda vya
Mega Trade na Pepsi mkoani hapa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka
10 ya bonanza hilo
0 comments:
Post a Comment