Nafasi Ya Matangazo

August 04, 2015

Maadhimisho ya siku ya mwanamke wa Afrika yanayoadhimishwa kila mwaka tarehe 31 July toka tamko rasmi la Umoja wa Afrika mnamo mwaka 1962 lililotolewa jijini Dar es Salaam -Tanzania.

WiLDAF Tanzania imekuwa ikiratibu maadhimisho haya hapa nchini ikiwa pia ni siku maalumu ya kusherehekea mafanikio ya wanawake wa Afrika. Katika maadhimisho hayo WiLDAF ilizindua ripoti ya kwanza ya hali za haki za Wanawake nchini Tanzania ya mwaka 2014 iliyozinduliwa na Mh. Anne Makinda, (SPIKA wa Bunge).

Maadhimisho haya yalifanyika siku ya ijumaa tarehe 31 July 2015 katika ukumbi wa Hyatt Regency Dar es Salaam.

Mgeni rasmi Mh. Anne makinda akiwasili ukumbini pamoja na mwenyekiti Mh Naomi Kaihula na mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya WiLDAF Edda Mariki, na mkurugenzi ?mtendanji wa WiLDAF Dkt Judith Odunga .

Mkurugenzi wa WiLDAF Dkt. Judith Odunga akimshukuru Mgeni rasmi Mh. Anne Makinda katika maadhimisho ya siku ya mwanamke wa Afrika.

Mgeni rasmi Mh. Anne Makinda akizindua ripoti ya hali za hali za wanawake nchini Tanzania ya mwaka 2014 iliyoandaliwa na WiLDAF

Mgeni rasmi Mh Anne Makinda akihutubia katika maadhimisho ya siku ya Wanawake wa Afrika iliyoandaliwa na WiLDAF

Washiriki kutoka mashirika mbalimbali wakifuatilia mada katika maadhimisho ya siku ya mwanamke wa afrika iliyoandaliwa na WiLDAF
Posted by MROKI On Tuesday, August 04, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo