Mkurugenzi Mtendaji
wa Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu nchini (Mjumita), Rahima Njaidi akizungumza wakati wa uzinduzi wa maazimio hayo ya wananchi kwa vyama vyama vya siasa nchini ambapo maazimio hayo yatakabidhiwa kwa vyama vyote vinavyoshiriki Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu utakao fanyika Oktoba 25, ili wakaweze kuzungumzia na kujibu maswali ya wananchi juu ya uhifadhi wa misitu na mazingira.
Mkurugenzi Mtendaji
wa Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu nchini (Mjumita), Rahima Njaidi akiendelea kuzungumza ambapo MJUMITA inawataka wagombea wa ngazi mbalimbali katika uchaguzi huuo pamoja na mambo mengine kuzungumzia juu ya uhifadhi wa mazingira katika mikutano yao hasa kutokana na umuhimu wa mazingira katika ustawi wa jamii na taifa kwa ujumla.
MJUMITA imesema Kumekuwa na desturi
ya baadhi ya wanasiasa kutoa kauli zinazokinzana na sheria na sera za misitu. Baadhi
ya wanasiasa wamekuwa wakitoa matamko na ahadi (hasa wakati wa uchaguzi) kwamba
kwa nafasi zao watashawishi shughuli za kibinadamu kuruhusiwa katika maeneo ya
hifadhi za misitu.
"Kauli za namna hiyo zimekuwa na athari kubwa kwenye juhudi
za uhifadhi wa misitu nchini ikiwa ni pamoja na baadhi ya misitu kuvamiwa na
wananchi. Wanamtandao tunataka serikali na viongozi watakaochaguliwa,".....:
- "Kukemea wanasiasa na viongozi wengine watakaotoa kauli zitakazokinzana na sera na sheria za misitu.
- Kuwachukulia hatua viongozi ambao kwa kauli na matendo yao wamesababisha kuvamiwa na kuharibiwa kwa misitu ya asili".
Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu nchini (MJUMITA),Rehema Ngelengele akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.
Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu nchini (MJUMITA),Rehema Ngelengele akizungumza. Kulia ni Kiongozi Mtetezi wa Jamii waishio kandokando ya Misitu (CAL), Revocatus Njau.
Wajumbe wakifuatilia.
Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu nchini (MJUMITA),Rehema Ngelengele (kulia) na Mkurugenzi wa Mjumita, Rahima Njaidi wakifuatilia mada wakati wa uwasilishaji wa Mazimio hayo.
Wajumbe na washiriki wakifuatilia mada katika mkutano huo.
Elias Monga, Meneja mradi akiwasilisha maazimio hayo ya wananchi kwa wajumbe wa Bodi ya Mjumita.
0 comments:
Post a Comment