Mabingwa
wa wapya wa Kombe la Kagame timu ya Azam FC wakishangilia na kombe lao
mara baada ya kukabidhiwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
leo.
Azam FC wameibuka mabingwa wa kombe hilo baada ya kuifunga timu ngumu ya Gor Mahia ya Kenya katika mchezo wa fainali kwa mabao 2-0. Azam imemal;iza michuano hiyo huku beki zake na mlinda mlango wao wakiwa hawajaruhusu goli hata moja katika lango lao kwa dakika 90 za mchezo.
Bao la kwanza la Azam lilifungwa kunako dakika ya 16, kupitia kwa John Bocco
‘Adebayor’ aliyeitendea haki krosi safi ya Kipre Tchetche.
Bao hilo lilidumu hadi kipindi
cha kwanza kinamalizika ambapo timu iliporudi uwanjanani zilecheza kwa
kushambukliana lakini bado nyota ilikuwa kwa watoto wa nyumbani Azam FC ambao
katika dakika ya 64, Kipre Tchetche akapachuika bao la pili lililodumu hadi
kipenga cha mwisho cha mwamuzi Louis
Hakizimana wa Rwanda
0 comments:
Post a Comment