MWANDISHI
wa habari ni mtu muhimu sana katika jamii, na wakati mwingine amekuwa
akitambulika kama Mhimili wa nne usio rasmi wa serilali, ukiacha Bunge,
Mahakama na Serikali.
Waandishi
wapo mstari wa mbele sana kuhamasisha jamii kushiriki katika shughuli za
maendeleo, kupaza sauti juu ya kero mbalimbali zilizopo katika jamii hizo na
hata watatuzi wa hizo kero ama serikali au makundi mengine katika jamii hizo
kuona na kutafuta ufumbuzi wake.
Mwandishi
wa habari ni mtu ambaye huitumia kalamu yake ama kujenga kitu au mtu na mtu
huyo ama kitu hicho kuonekana ni bora zaidi kuliko vyote lakini pia kalamu hiyo
hiyo Mwandishi anaweza kuitumia kuboa kabisa kile alichokijenga kwa sifa nyingi
na jamii kuona huyu ndio mtu.
Hebu
ona sasa hivi mwandishi wa habari hasa yule anayeaminika katika chumba fulani
cha habari alivyo ‘lulu’ katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa
Rais, Wabunge na madiwani.
Kila
mtu mwenye nia ya kutaka kugombea kuwania moja ya nafasi za uongozi anahaha
kupata mwandishi ambaye kama si kuamuandika vizuri gazetini au kumtangaza
vizuri na hao wapiga kura wake watarajiwa wakamsoma ili wamchague.
Ndio!
Na waandishi wa wazuri wapo wengi sasa wadau hapa wanazidiana kete tu na mtu
kutoka huku kwenda huku. Wapo wanaofanya kazi hiyo ya kuwapamba na kuwafagilia
watu ilimradi tu aione kesho yake bila kujadi maadili au laa lakini wapo wanaoifanya kazi hiyo kwa
kuzingatia maadili.
Mwandishi
wa habari amekuwa mbele sana katika kufanya mambo ya watu, lakini akijisahau
yeye mwenye matatizo lukuki yanayo mkabili. Hebu angalia wafanyakazi wa kampuni
fulani wagome kuhusiana na maslahi duni wanayopata au manyanyaso kwa mwajiri
wao uone kesho watakavyo andika magazetini na kutangaza, lakini wamesahau kuwa
wao ndio watu wa mwisho katika maslahi na hata hayo madogo wanayotakiwa
kuyapata hawayapati kwa wakati.
Hivi
sisi waandishi tumelogwa! Na kama ndio basi aliyetuloga hiyo tunguli kaitupa
baharini na na mganga mwenye kujua tiba yake kafa. Haiwezekani tumeshindwa
kujikingia kifua, ni waoga au nini kinatusibu hata kushindwa kupigania maslahi
yetu? Jamani haya maslahi tunashindwa hata kusaidiana nako tunashindwa?SOMA ZAIDI HAPA
Ni ukweli usiopingika, inatakiwa kuamka, kusimama pamoja na kuwa na sauti moja
ReplyDelete