Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni
Sefue akisikiliza na kufurahia maelezo kutoka kwa Bi Martha Mashiku, Afisa
Masoko na Mawasiliano Mwandamizi UTT AMIS(katikati), Kushoto ni bi Sophia Mgaya
afisa mwandamizi kitengo cha Tehama na Kulia ni Bi Jesca Swai, Mhasibu wa Mifuko inayoendeshwa na UTT AMIS.
*******************
MIFUKO ya uwekezaji wa pamoja
ni fursa mbadala inayowezasha watu ,vikundi,taasisi na kampuni sawa na mahitaji
yao kuwekeza pesa zao kwa meneja wa mfuko(UTT AMIS) kisha meneja huwekeza fedha
hizo katika masoko ya fedha na masoko ya mitaji kulingana na waraka wa
makubaliono. Faida ipatikanayo hugawanywa kwa wawekezaji kulingana na uwiano wa
uwekezaji waliofanya katika mfuko husika.
Mpaka sasa UTT AMIS inaendesha mifuko mitano
ambayo ni Mfuko wa Umoja, Mfuko wa Wekeza Maisha, Mfuko wa Watoto, Mfuko wa
Kujikimu na Mfuko wa Ukwasi yenye jumla ya thamani ya Zaidi ya Shilingi bilioni
237.
Mifuko yote hii imeweza kukidhi vigezo muhimu vya uwekezaji ambavyo ni Usalama,Ukwasi na Faida (Safety,
Liquidity and Returns). Wawekezaji
wote wananufaika kwa kupata faida
shindani, uwekezaji mseto hufanyika ili kupunguza hatari za uwekezaji,utalaamu
wa meneja wa mifuko,unafuu wa mkubwa wa gharama na uwazi kwani bei halisi ya
vipande vya mifuko hutangazwa kila siku za kazi.
Hapa ni rahisi
tuu!!Afisa Masoko na Uhusiano msaidizi Bw. Waziri Ramadhani akimuelekeza
mwekezaji jinsi ya kujaza fomu ya kujiunga katika moja ya mifuko ya uwekezaji
ya UTT AMIS
Tunaweza kuwasaidia kujaza fomu zenu!
Bi. Pauline Kasilati na Dorice Mlenge Ofisa wasaidizi wakitoa huduma kwa
wawekezaji kwa kuwasaidia kujaza fomu za kujiunga na Mfuko wa Watoto
Laurian Chokola, Afisa mwendeshaji msaidizi
akiwaelekeza wawekezaji kujaza fomu za kujiunga na mifuko baada ya kuwaelimisha
faida zinazopatikana kwa kuwekeza kwenye mifuko ya uwekezaji wa pamoja.
0 comments:
Post a Comment