Kamanda
wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina Suleiman Kova
akionyesha bunduki zilizoporwa katika uvamizi wa uliofanywa na majambazi
katika kituo stakishari,Tazara leo jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina Suleiman
Kova akionyesha Fedha taslimu Sh.Milioni 170 zilizkutwa katika Shimo na
majambazi waliovyamia kituoa stakishaari na kuua askari,leo jijiji Dar
es Salaam.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
JESHI
la Polisi Kanda ajijini Dar es salaam limefanikiwa kuwatia mbarini Watu
wawili wanaotuhumiwa kuwa Majambazi waliovamia Kituo cha Polisi
Stakishari, Ukonga jijini Dar es Salaam, huku wengine watatu wakiwa
wameuwawa katika shambulio la kutupiana risasi katika eneo la Tuangoma,
Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Tukio
hilo la kukamatwa na kuuawa kwa majambazi hao lilitokea Julai 17 mwaka
huu huko maeneo ya Tuangoma Kigamboni jijini Dar es Salaam, na majambazi
wa tukio la kinyama la kuuwawa kwa askari wanne na raia watatu katika
kituo cha Stakishari wanakadiriwa kuwa kati ya 16 hadi 18.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Kamanda wa Polisi wa
Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina Suleiman Kova amesema kukamatwa
kwa majambazi hao inatokana na kikosi kazi kilichoundwa na kanda
maalumu kwa kushirikia na Mkoa Pwani.
Kamanda
wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Suleiman Kova akizungumza na
waandishi wa habari kuhusu kukamatwa kwa watuhumiwa wa ujambazi
waliovamia kituo cha Polisi cha Stakishari, Tazara,leo jijini Dar es
Salaam.
Naibu
wa Kamshina wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Simon Sirro akizungumza na
waandishi wa habari juu operesheni iliyofanyika ya kuwakamata
watuhumiwa wa ujambazi waliovyamia kituo cha Stakishari ,Tazara,jijini
Dar es Salaam. SOMA ZAIDI HAPA
0 comments:
Post a Comment