Nafasi Ya Matangazo

July 10, 2015


Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya  Kikwete akiongoza kikao maalum cha kamati kuu ya CCM katika ukumbi wa White House mjini Dodoma leo. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti Zanzibar ambaye pia ni Rais wa SMZ Dk Ali Mohamed Shein, Makamu Mwenyekiti Bara Ndugu Philip Mangula (kulia) na  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.

Habari kutoka Dodoma ambako mkutano Mkutano wa CCM wa kutafuta mgombea wake unaendelea zinaarifu kuwa Kamati Kuu (CC) bado inaendelea.

Aidha habari kutoka mjini humo zinapasha kuwa Mkutano wa Halmashauri Kuu (NEC) ambao unajumuisha wajumbe 378 uliokuwa ukutane baada ya kumalizika CC huenda ukafanyika kesho saa 4 asubhi na ule Mkutano Mkuu ukafanyika saa 8 jioni.

Kamati Kuu inaendelea na mchakato wa kupata wagombea 5 ambao wanatakiwa kuingia NEC kujadiliwa na kasha kutoa majina matatu yatakayoenda kupigiwa kura Mkutano Mkuu kesho.

Rais Mstaafu awamu ya pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Rais Mstaafu awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa,wakiongea kabla ya kuanza kwa kikao
 Baadhi ya wajumbe wa kikao maalum cha Kamati kuu ya CCM kutoka kushoto ni Rais Mstaafu awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa, Makamu mwenyekiti Bara Mstaafu Ndugu Pius Msekwa, Rais Mstaafu Zanzibar Ndugu Amani Abeid Karume, Mawaziri Mkuu wastaafu Cleopa David Msuya na Salim Ahmed Salim
Posted by MROKI On Friday, July 10, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo