Nafasi Ya Matangazo

July 11, 2015

Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete akizungumza wakati wa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) katika ukumbi wa Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma jana. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Visiwani na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.

Pamoja na mambo mengine pia itapitisha majina 3 ya wagombea urais kupitia CCM na baade kuyapeleka majina hayo Mkutano Mkuu lakini pia ina fanya marekebisho ya katiba yake juu ya wagombea wa Viti maalum kufutiwa ukomo na kupokea ilani ya Chama Cha Mapinduzi.
SIASA SIO UADUI.... Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kushoto) akisaliamana huku wakiwa ni wenye furaha na  Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa baada ya kuteuliwa kuingia katika tano bora ya wawania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, kabla ya kuanza kwa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) katika ukumbi wa Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma jana.
Baadhi ya Wajumbe wa kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) (NEC) wakisalimiana na kumpongeza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kulia), baada ya kuteuliwa kuingia katika tano bora ya wawania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, kabla ya kuanza kwa kikao cha NEC, katika ukumbi wa Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma jana.
Posted by MROKI On Saturday, July 11, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo