Nafasi Ya Matangazo

July 07, 2015

Mkurugenzi Mkuu wa michezo ya Bodi ya michezo ya kubahatisha nchini Tarimba Abbasi akiteta jambo na Mwenyekiti wa michezo ya kubahatisha ya Gidan International Profesa , Bongani Aug Khumalo wakati wa utoaji wa elimu kwa wananchi waliofika kwenye banda hilo lililopo kwenye  maonyesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam juu ya michezo ya kubahatisha itakayozinduliwa baadaye mwaka huu.
Mkurugenzi Mkuu wa michezo ya Bodi ya michezo ya kubahatisha nchini Tarimba Abbasi (kushoto) akikabidhiwa tiketi ya bahati nasibu na  Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya Gidani International, Clive Reynofrs wakati wa uzinduzi wa mchezo huo uliofanyika kwenye viwanja vya maonyesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam(Sabasaba) Wa pili kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa kampuni ya Gidani International Profesa , Bongani Aug Khumalo na Mkurugenzi mwendeshaji wa kampuni hiyo Brett Smith.
Mwenyekiti wa  Kampuni ya michezo ya kubahatisha ya Gidani International  yenye makao yake makuu nchini Afrika ya Kusini, Profesa  Bongani Aug Khumalo akiwaelimisha wananchi waliofika kwenye banda la Michezo ya kubahatisha lililopo kwenye maonesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam, (Sabasaba)  jinsi michezo itakayochezeshwa na kampuni hiyo itakavyoendeshwa.
Mwenyekiti wa bodi ya michezo ya kubahatisha nchini Bw. Wiliam Mdundo (katikati) akiwahamasisha wananchi waliofika kwenye banda la bodi hiyo liliopo kwenye maonesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam, (Sabasaba) ili waweze kushiriki katika michezo  ya   bahati nasibu  inayotarajiwa kuzinduliwa nchini mwezi Novemba na kampuni ya Gidani International.Kushoto ni Mwenyekiti wa  Kampuni hiyo Profesa , Bongani Aug Khumalo
Mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni ya Michezo ya Kubahatisha ya Gidani International akitoa elimu kwa wananchi waliofika kwenye banda hilo lilopo kwenye maonesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam(Sabasaba)  juu ya elimu ya mchezo huo utakaozinduliwa mwezi Novemba ambapo washiriki watajinyakulia zawadi mbalimbali akiwemo mshindi wa zawadi kubwa ya kitita cha shilingi  bilioni 1.
Mwenyekiti wa  Kapuni ya michezo ya kubahatisha ya Gidan Intarnationa  Profesa , Bongani Aug Khumalo (mwenye shati nyeusi) akiwa katika ya pamoja na wafanyakazi wa Bodi ya michezo ya akaubahatisha Tanzania wakati wa uzinduzi wa mchezo huu uliofanyika kwenye maonesho ya maonesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam, (Sabasaba) Bahati na sibu yaTaifa unarajiwa kuzinduliwa rasmi mwezi November 2015.
Posted by MROKI On Tuesday, July 07, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo