Meneja wa Mfuko Mkoa wa Lindi Fortunata Raymond akifafanua
dhamira ya mfuko katika kuleta mabadiliko kwenye sekta ya afya,kupitia mikopo
iliyoboreshwa ,kwani hadi kufikia mwezi mei.2015 watoa huduma wa mkoa wa Lindi wameweza kukopa
takribani 135mil.ambapo kati ya fedha hizo hospitali ya mkoa ilikopa ultra
sound yenye thamani ya 54Mil.amesisitiza kuwa huduma zinapoimarika hususani upatikanaji wa dawa wananchi
hawatasisita kuchangia kwenye CHF.
Kaimu katibu tawala wa Mkoa wa
Lindi Grayson Mwaigombe amewataka
waganga wakuu wa hospitali kuanzia ya mkoa na wilaya,kuchangamkia mikopo
ya riba nafuu inayotolewa na NHIF,ili waweze kuboresha huduma na pia kuwa
chanzo kingine cha mapato ya hospitali,kwani wananchi kwa sasa wanahitaji
huduma bora na stahiki,aliyesema hayo wakati wa elimu ya uhamasishaji watoa
huduma wa Serikali, mashirika ya dini na watu binafsi waliosajiliwa na
mfuko,kuchangamkia fursa ya mikopo ya vifaa tiba,ukarabati wa maeneo ya kutolea
huduma ,dawa na vitendanishi,Mkoani Lindi leo kwenye ukumbi wa mikutano wa
hospitali ya sokoine.
Mtoa elimu afisa kutoka makao makuu ya mfuko Isaya
shekifu akiwasilisha mada inayotoa miongozo na taratibu za maombi ya
mikopo,ambapo aliwataka watoa maamuzi kutoa kipaumbele katika kuboresha huduma
za matibabu kwani kutachochea wananchi wengi kujiunga na CHF, hivyo kuongeza
mapato ya hospitali,kwa sasa mfuko umetenga jumla ya 2bilioni ili watoa huduma
wa serikali,binafsi na mashirika ya dini waweze kukopa.
Washiriki
wa mafunzo hayo ambayo yaliwajumuisha viongozi wa halmashauri Lindi na waganga wakuu
na wenyeviti wa halmashauri,watoa huduma wa binafisi wakimsikiliza mgeni rasmi
kaimu katibu tawala hayupo pichani.
Mganga mfawidhi kituo cha afya mjini kati Lindi Dr. Zulfa Msami akiuliza jambo baada ya uwasilishwaji wa mada.
0 comments:
Post a Comment