Hawa ni miongoni mwa Watanzania waliohamasika kutembelea katika viwanja vilivyokuwa kwenye mradi wa Vikuruti kutoka Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, wilayani Kibaha, mkoani Pwani, ambavyo vinatolewa kwa wananchi kwa mkopo. Wakopaji ni watumishi wa umma, kampuni binafsi na wajasiriamali.
Eneo la viwanja vya Vikuruti vinavyoonekana huku barabara ikionekana pichani.
**********
Na Mwandishi
Wetu, Dar es Salaam
WATANZANIA
wameendelea kuvichangamkia viwanja vya mkopo vinavyotolewa na Taasisi ya
Kifedha ya Bayport Financial Services, vilivyopo Vikuruti, wilayani Kibaha,
mkoani Pwani.
Kuchangamkiwa
kwa viwanja hivyo kumekuja siku chache baada ya kuzindua huduma mpya ya mikopo
ya viwanja hivyo kutoka Bayport, ikiwa ni ishara nzuri na njia ya kuwapa fursa
Watanzania ya kumiliki nyumba.
Akizungumza
jana jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial
Services, Ngula Cheyo, alisema watu wengi wamekuwa wakituma maombi ya kuomba
kupewa viwanja hivyo, tangu huduma hiyo ilipozinduliwa rasmi.
Alisema
kwamba baadhi ya watu walioonyesha nia ya kuvipata viwanja hivyo pamoja na
kutuma maombi yao, pia wamekuwa wakitembelea eneo kulipokuwa na viwanja hivyo
ili wajiridhishe kwa ajili ya kujipatia viwanja hivyo vinavyokopeshwa kwa
minajiri ya kuwakwamua Watanzania, ukizingatia kuwa ardhi inapanda thamani siku
hadi siku.
“Jana (juzi)
zaidi ya watu 82 wamekwenda Vikuruti, Kibaha kujionea eneo lenyewe na kuchagua
viwanja wapendavyo, ikiwa ni mwendelezo mkubwa wa wananchi wanaotuma maombi ya
kukopa viwanja vya Bayport, wakichukua fomu bure z kwa kupitia matawi yetu yaliyoenea nchi
nzima, bila kusahau kwenye matawi ya Bank of Afrika (BOA).
“Huduma hii
ni murua kwa Watanzania wote, tukiamini kuwa ni sehemu ya kuwapatia wananchi
urahisi wa kumiliki vitu vyenye thamani ikiwamo ardhi wanayoweza kuitumia kwa
mambo mengi, ikiwa nyumba za kuishi na za biashara, huku thamani ya viwanja
vikianzia Sh 1,400,000 na kuendelea kwa viwanja vyenye ukubwa tofauti vya
kujenga nyumba za kuishi na biashara kama vile shule, vituo vya afya, nyumba za
kulala wageni na hoteli,” alisema Cheyo.
Cheyo
alisema nafasi ni chache, maana maombi yanafanyika kwa siku (20), kuanzia Mei
22 hadi Juni 10, huku fomu za maombi zikipatikana katika matawi yao yote ya
Bayport Financial Services na matawi ya bank of Africa (BOA), ambapo malipo ya
awali yakianzia Sh 150,000 na yatakuwa yakilipwa kwa akaunti yao ya Bayport
iliyopo BOA.
Kwa mujibu
wa Cheyo, fomu ya maombi na nakala ya malipo ya awali yarejeshwe katika matawi
BOA au ofisi za taasisi ya Bayport zilizoenea nchi nzima na baada ya Juni 10,
mteja atatakiwa kulipia kiwanja kwa fedha taslimu au mkopo kutoka kwenye
taasisi yao huku watumishi wa umma na wa kampuni binafsi wakiweza kukopeshwa
kiwanja na kukabidhiwa hati miliki ndani ya siku (90) watakapokamilisha mkopo
wao.
0 comments:
Post a Comment