Ofisa Mafunzo Idara ya Masoko UTT AMIS, Waziri Ramadhani (kulia) akitoa maelezo ya namna ya kujiunga na Mfuko
wa Umoja wakati wa maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Ofisa Mafunzo Idara ya Masoko UTT AMIS, Waziri Ramadhani (kulia) akitoa maelezo ya namna ya kujiunga na Mfuko
wa Umoja wakati wa maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Kulia ni Ofisa wa Mafunzo wa UTT AMIS, Doris Malenge.
Mmoja wa Wateja waliotembelea banda la UTT AMIS akijaza fomu kwa ajili ya Mfuko wa Watoto kwenye maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma jijini Dar es Salaam. Kulia ni Ofisa Msaidizi wa Huduma kwa Wateja, Saidi Mkomwa.
Maofisa wa UTT AMIS wakiwa katika picha ya pamoja. Wa pili kulia ni Ofisa Masoko Mwandamizi, Martha Mashiku, kulia ni Ofisa Msaidizi wa Huduma kwa Wateja, Saidi Mkomwa, Ofisa Uendeshaji UTT AMIS, Justine Joseph (kushoto) na Ofisa Mafunzo, Doris Mlenge (wa pili kushoto) na Ofisa Mafunzo Idara ya Masoko, Waziri Ramadhani (katikati).
*******
Kampuni ya Uwekezaji ya UTT Asset Management and Inventor
Services Plc (UTT AMIS) ni mrithi wa taasisi ambayo hapo awali ilijulikana kama Dhamana ya Uwekezaji Tanzania (UTT),
ambayoiliundwa Juni 19, 2003.
UTT AMIS ni taasisi ya serikali chini ya Wizara ya Fedha
ambayo kuanzia mwezi Julai 2013 imechukua na kusimamia kazi zote za iliyokuwa
UTT.
Dhumuni kuu ni kuazisha na kuendesha mifuko ya uwekezaji wa
pamoja ili kuwawezesha wananchi kujiwekea akiba huku wakiwekeza katika Masoko
ya Mitaji na Fedha. Hadi sasa UTT AMIS inaendesha mifuko mitano, ambayo ni Mfuko
wa Umoja, Mfuko wa Wekeza Maisha, Mfuko wa Watoto, Mfuko wa Kujikimu na Mfuko
wa Ukwasi.
0 comments:
Post a Comment