Jokate (kushoto) akizungumza katika mkutano wa
jukwaa la sanaa. Katikati ni katibu mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Sanaa na Utamaduni
nchini, (CAJAtz), Hassan Bumbuli na mbunifu mkongwe wa mavazi, Asia Idarous.
****************
Na Mwandishi wetu
Msichana mwenye vipaji lukuki nchini, Jokate Mwegelo
amewataka wasanii kuwa wabunifu ili kupata mafanikio katika sanaa na shughuli
zao za kila siku.
Jokate alitoa wito huo wakati akitoa mada katika
Jukwaa la Sanaa la lililoandaliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kwa kushirikiana
na chama cha Waandishi wa Habari za Sanaa
na Utamaduni nchini, (CAJAtz).
Alisema kuwa sanaa ina wigo mpana sana na kila
msanii anatakiwa kuwa mbunifu ili kujiweka tofauti na msanii mwingine na kujipatia fedha kwa
kutumia ubunifu wake.
Kwa mujibu wa Jokate, yeye aliamua kupitia kwenye
fani ya urembo na mwaka 2006 alifanikiwa kushika nafasi ya pili katika
mashindano ya Miss Tanzania. Alisema kuwa aliamua kutumia umaarufu wake
kujipatia maendeleo pamoja na ukweli kuwa alisomea mambo ya siasa Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam.
“Elimu yangu ya mamo ya siasa haina nafasi kwangu,
nilianza kuwa mshehereshaji (MC) katika shughuli mbalimbali, nikaingia katika
fani ya ubunifu wa mabavi (Kidoti Fashion), nikaanzisha kidoti club ili kupata
marafiki ambao tutazungumza lugha moja,” alisema Jokate.
Mrembo huyo hakuishia hapo kwa kuingia katika fani
ya utangazaji wa vipndi hasa Chanel O, uigizaji wa filamu, utengenezaji wa
nywele, ndala na sasa mwanamuziki.
“Hii yote ni
kutafuta ‘chaneli’ za kupata fedha, nimefanikiwa na sasa nina makubaliano yenye
thamani ya Sh 8.5 bilioni na kampuni ya Kichina, Rainbow Shell Craft Company
Limited kwa ajili ya kuzalisha na kuuza bidhaa mbalimbali za lebo yake ya
Kidoti,” alisema.
Mbali ya Jokate, mbunifu maarufu nchini, Asia
Idarous naye aliwataka wasanii kuwa waaminifu na kujitangaza katika shughuli
zao ili kupata maendeleo.
Idarous
alisema kuwa msanii ambaye atakuwa mbunifu na kipaji cha hali ya juu,
hataweza kupata maendeleo kama atakosa sifa ya uaminifu ambayo mara nyingi
uendana na nidhamu katika kazi.
“Mimi nilianza kazi ya ubunifu wa mavazi miaka ya
1980, mpaka leo nafanya kazi hii, wabunifu wengi (hata Jokate) amepitia kwangu,
siri kubwa ya mafanikio haya ni uaminifu na nidhamu katika kazi, nimefanikiwa
kuanzisha Vazi la Khanga nchini Marekani na Lady in Red, leo hii ni maarufu,”
alisema Idarous.
Katibu Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Sanaa na Utamaduni
nchini, (CAJAtz), Hassan Bumbuli alitoa wito kwa wasanii chipukizi kufuata
nyayo za Jokate na Idarous ili kuweza kufanikiwa katika kazi zao za sanaa.
Bumbuli alisema kuwa ni vigumu kupata mafanikio
katika sanaa bila kuweka wazi kipaji chako hadharani na hapo ndipo vyombo vya
habari vitakuona na kuanza kuandika habari zao.
0 comments:
Post a Comment