Mmoja wa Wakurugenzi wa Kampuni ya Masoko inayojihusisha na masuala ya mawasiliano na masoko, Conctantine Magavila (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati wa uzinduzi wa kampeni maalumu ya kuhamasisha vijana kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura na hatimaye kupiga kura ilijulikanayo kama 'Kuradili". Kampuni hiyo itafanya kampeni hiyo katika mikoa kadhaa kwa kushiriakiana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Shirika la Open Society International East Africa (OSIEA), pamoja na wasanii mbalimbali wa muziki. Kulia ni mwanamuziki Sinura Mushi na kushoto ni Ofisa Elimu Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Rose Malo.
Mmoja wa Wakurugenzi wa Kampuni ya Masoko inayojihusisha na masuala ya mawasiliano na masoko, Conctantine Magavila (katikati), akizungumza katika mkutano huo. Kutoka kulia ni Mwanamuziki Stamina, Kala Jeremia, Snura, Ofisa Elimu Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Rose Malo na Ofisa Mipango Msaidizi wa Shirika la Open Society International East Africa (OSIEA), Adam Anthony.
Mkutano ukiendelea.
Wanamuziki wakiwa kwenye mkutano huo. Kutoka kulia ni Stamina, Kala Jeremia, na Snura.
**************
**************
Na
Dotto Mwaibale
KAMPUNI ya Masoko inayojihusisha na masuala ya mawasiliano na masoko kwa
kushirikiana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na shirika la Open
Society International East Africa (OSIEA) na wasanii mbalimbali wa muziki
wamezindua kampeni maalumu ya kuwahamasisha vijana kujiandikisha katika
daftari la kudumu la wapiga kura na hatimaye kupiga kura.
Kampeni
hiyo iliyozinduliwa Jijini Dar es Salaam leo inatarajiwa kuhusisha mikoa mitano ikiwemo Dar es Salaam, Morogoro, Mwanza,Shinyanga na
Morogoro ambapo yatafanyika matamasha mbalimbali ambayo hayana
viingilio na yatakayowahusisha wasanii walioteuliwa kama mabalozi katika
kampeni hii.
Kauli
mbiu ya kampeni hii ni ‘Kura dili’ na lengo kuu ni kuhakikisha vijana
wengi iwezekanavyo wanajiandikisha na kujitokeza kwa wingi kupiga kura.
Wasanii
watano wametunga wimbo maalumu uitwao ‘Kuradili ambao pia ulizinduliwa
katika hafla hiyo na utatumika katika kampeni hii.
Wasanii
hao ni pamoja na Gnako, Snura, Izo Biznez, Kala Jeremiah na Stamina.
Akizungumza
kwa niaba ya Masoko,mmoja wa wakurugenzi, Constantine Magavila alisema
kampeni hiyo inalenga kuwafikia zaidi ya watu milioni 4 kujisajili na
kupiga kura na watashirikiana na redio mbalimbali kuhakikisha wimbo huo maalumu
unapigwa katika redio mbalimbali ili kuhamasisha zaidi.
0 comments:
Post a Comment