MBUNGE wa Bumbuki CCM na Naibu Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia January Makamba ametangaza nia kwa mara nyingine ya kuwania urais akiahidi
serikali yake kuunda baraza la mawaziri wasiozidi 18 wasiotiliwa shaka
na wananchi juu ya uwezo na uadilifu wao.
Makamba ambaye alishatangaza nia hiyo mwaka jana
akiwa London, Uingereza alisema ametafakari kwa kina kuhusu changamoto
zinazoikabili nchi na aina mpya ya uongozi inayohitajika na kuamua
kuomba ridhaa ya urais ili azitatue.
Mwanasiasa huyo aliwaambia wananchi waliojitokeza
kumsikiliza kuwa kesho atakwenda Dodoma kuchukua fomu ya kuomba ridhaa
hiyo na kuongeza kuwa; “sijagombea kugombana na watu, nimegombea
kupambana na changamoto za watu. Naiomba nafasi huku nikielewa kiu ya
Watanzania kupata aina mpya ya uongozi wa zama za sasa utakaotoa
matumaini mapya yatakayozaa Tanzania mpya. Naelewa misingi iliyojenga
nchi yetu ya haki, umoja, amani na upendo na mshikamano… inayotakiwa
kulindwa kwa gharama zote.”
Alisema aina ya uongozi wa utakaochaguliwa Oktoba
ndiyo utakaoamua mustakabali wa nchi na majawabu mapya
yatakayomtofautisha yeye na wengine.
Makamba ambaye aliyohutubia kwa takribani saa
1.17, alisema atainadi ilani ya CCM kwa nguvu zote na serikali
atakayounda itaongozwa na falsafa ya uwezeshaji mpana kwa wananchi
kisiasa, kiuchumi na kijamii.
“Sitaunda serikali ya waporaji na wabinafsi.
Nitaunda serikali yenye utu, inayowasikiliza watu, itakayotimiza wajibu
wake bila chembe ya uonevu wala ulegevu… nitaunda serikali ya mawaziri
18 ambayo haitakuwa na mtu hata mmoja anayetiliwa shaka uadilifu wake au
uwezo wake,” alisema Makamba huku akishangiliwa.
Alisema serikali yake itakuja na vipaumbele vitano
vya kukuza vipato vya watu kwa shughuli zote, huduma bora na za uhakika
za kijamii; utawala bora, haki, utawala wa sheria, usimamizi wa uchumi
na kulinda amani, umoja na usalama wa nchi.
Makamba (41) alieleza namna atakavyotekeleza
vipaumbele vyake kama alivyokwisha eleza katika mahojiano yake yaliyomo
katika kitabu cha Padri Privatus Karugendo kiitwacho Maswali na Majibu
40 juu ya Tanzania Mpya.
Kuhusu ukuzaji wa uchumi, mbunge huyo wa Bumbuli
alisema ataunda baraza la uchumi litakalojumuisha wataalamu kutoka
taasisi za umma, magwiji wa uchumi na wawakilishi wa sekta binafsi,
litakalohakikisha uchumi unawekewa mipango ya muda mfupi na mrefu
kutatua changamoto zinazoikabili nchi.
Soma zaidi MWANANCHI
Soma zaidi MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment