Aliyekuwa
Balozi wa Kudumu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Augustine Mahiga akizungumza
wakati akitangaza nia ya kugombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania leo katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dar es
Salaam. kushoto ni Mke wa Aliyekuwa Balozi wa Kudumu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Augustine Mahiga, BI Elizabeth Julius Mahiga.
Baadhi
ya waandishi wa habari na wananchi wakimsikiliza
Balozi wa Kudumu wa Umoja wa Mataifa,Dk Augustine Mahiga wakati
akitangaza nia ya kugombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania jijini Dar es Salaam leo.
*************
ALIYEKUWA
Balozi wa Kudumu wa Umoja wa Mataifa,Dk. Augustine Mahiga ametangaza
nia ya kugombea urais ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), jijini Dar es
salaam leo.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini
Dar es Salaam, Mahiga amesema maadili yamemomonyoka na kufanya kuwepo
kwa rushwa na ufisadi.
Mahiga
amesema ubadhirifu na ufisadi katika taifa kunahitajika kuwepo kwa
mwelekeo katika kuweza kupambana na vitu hivyo ili maendeleo yapatikane
kwa wananchi.
“Nikipata
nafasi hii nitatumikia watu katika kuujenga uchumi imara kwa kila
mwananchi kutokana na kuwepo kwa dira na kuondoa matabaka yanayotokana
na ubadhirifu wa mali za umma”amesema Mahiga.
Amesema
CCM itoe fursa, isifikie utawala wa watu wenye pesa hiyo sio dhamira ya
CCM, na watu wanaotoa msaada uwe na kikomo chake.
Mahiga
amesema katika kuweza kufikia uchumi wa kati kunatakiwa kupambana na
rushwa na ufisadi, bila kufanya hivyo uchumi huo hautafikiwa.
0 comments:
Post a Comment