Aliyewahi kuwania jimbo la Arumeru Mashariki kupitia CCM Sioi Sumari akijinadi mbele ya Waziri
mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha Edward Lowassa
katika harambee ya kuchangia ujenzi wa msikiti wa Patandi ambapo Mh.
Lowassa alikuwa mgeni rasmi(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
Mbunge wa Viti Maalum, Namelock Sokoine akinadaiwa na Waziri
mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha Edward Lowassa
katika harambee ya kuchangia ujenzi wa msikiti wa Patandi ambapo Mh.
Lowassa alikuwa mgeni rasmi
*****
Baadhi
ya wagombea waliotangaza nia kuwania ubunge katika majimbo mbalimbali
mkoani Arusha kupitia CCM juzi walionekana kupigana vikumbo na wengine
wakijinadi mbele ya waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli
mkoani hapa Edward Lowassa.
Lowasa,ambaye
anatajwa kuwania urais kupitia CCM mwaka huu mwishoni mwa wiki
iliyopita aliendesha harambee ya ujenzi wa msikiti wa Patandi uliopo
wilayani Arumeru mkoani Arusha akimwakilisha makanu wa Rais,Dk Mohammed
Billal na kufanikiwa kukusanya zaidi ya kiasi cha sh,235 milioni ikiwa
ni zaidi ya makisio ya msikiti huo kukusanya sh,200 milioni .
Baadhi
ya watia nia wa CCM walionekana wakichangia fedha katika harambee hiyo
huku wengine wakitumia mwanya wa kunadi sera pindi walipokaribishwa
jukwaa kuu.
Wagombea
hao watarajiwa wa ubunge ni Mustapha Panju alitoa Sh6 milioni, Sioi
Sumari (Sh7 milioni), Kim Fute (Sh3 milioni), Philemon Mollel (Sh5
milioni), mbunge Peter Serukamba (Sh3 milioni) na mjumbe wa NEC kutoka
jimbo la Busega, Dk Raphael Chegeni alichanga Sh1 milioni sawa na mbunge
wa Arusha Mjini, Godbless Lema na Namelock Sokoine.
Hatahivyo,wakati
wagombea hao kwa nyakati tofauti mara walipofika kuchangia harambee
hiyo na kupewa nafasi ya kusema neno ndipo badhi yao walisikika wakinadi
sera kitendo kilichopelekea kuibua shangwe kwa wahudhuriaji.
Mke
wa mtia nia wa CCM,Violet Mfuko ambaye mmewe ametangaza nia,Kim Fute
alifika jukwaa kuu na kumnadi mmewe kwa kumwambia Lowasa kwamba
ametangaza nia na kuwataka makada wa CCM kumuunga mkono.
“Mheshimiwa
waziri mkuu mme wangu ametangaza nia jimbo la Arusha mjini,mimi ni mke
wake nawaomba jamani mumuunge mkono”alisema Mfuko na kuibua shangwe
Hatahivyo,mtia
nia mwingine wa CCM jimbo la Monduli mkoani Arusha,Sokoine naye
alipopanda jukwaani Lowasa alitumia nafasi hiyo kumnadi kwa kuwataka
makada wa CCM kumuombea kwa Mungu mambo yake yaende vizuri.
“Jamani huyu naye ametangaza nia huko Monduli tumuombee kwa Mungu mambo yake yaende vizuri “alisema Lowasa
Hatahivyo,Sumari,Monaban,Panju
na baadhi ya wagombea wengine walipanda jukwaa kuu na kisha
kujitambulisha kabla ya kuchangia fedha huku wakitamka ya kwamba
wanaomba mambo yao yaende vizuri ili wapitishwe kugombea ndani ya CCM.
0 comments:
Post a Comment