Nafasi Ya Matangazo

May 01, 2015



Makamu wa Rais wa kampuni ya StarTimes Tanzania, Zuhura Hanif (kulia) akimuelekeza mshindi wa droo ya tatu ya mwezi wa Aprili, Mary Luis Tumsifu, mfanyabiashara wa vyakula vya mifugo na mfugaji pia, mkazi wa Kijitonyama jijini Dar es Salaam namna ya kuchomeka ufunguo wa pikipiki katika hafla fupi iliyofanyika katika duka la kampuni hiyo zilizopo Bamaga-Mikocheni jijini Dar es Salaam leo. Kujiunga na bahati nasibu hiyo wateja wa StarTimes wanatakiwa kulipia kifurushi kuanzia shilingi 10,000/- na kuendelea.


Makamu wa Rais wa kampuni ya StarTimes Tanzania,  Zuhura Hanif (kulia) akimkabidhi mshindi wa simu ya kisasa aina ya Solar 5,  Richard John, mkazi wa Mwananyamala jijini Dar es Salaam mara baada ya kuibuka mshindi wa droo hiyo ya  tatu ya kujishindia pikipiki na simu ya mwezi wa Aprili inayoendeshwa na kampuni hiyo. Katikati akishuhudia ni Bw. Gideon Fumbuka ambaye naye alijinyakulia simu kisasa aina ya P40. Kujiunga na bahati nasibu hiyo wateja wa StarTimes wanatakiwa kulipia kifurushi kuanzia shilingi 10,000/- na kuendelea.  
Mshindi wa droo ya bahati nasibu ya kujishindia pikipiki inayoendeshwa mwezi huu wa Aprili na StarTimes Tanzania, Mary Luis Tumsifu, mfanyabiashara wa vyakula vya mifugo na mfugaji pia, mkazi wa Kijitonyama, jijini Dar es Salaam  akionyesha nyaraka za pikipiki kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kukabidhiwa katika ofisi za kampuni jijini Dar es Salaam. Pamoja naye katika makabidhiano ni Makamu wa Rais wa kampuni ya StarTimes Tanzania, Zuhura Hanif, kujiunga na bahati nasibu hiyo wateja wa StarTimes wanatakiwa kulipia kifurushi kuanzia shilingi 10,000/- na kuendelea.


Posted by MROKI On Friday, May 01, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo