Mwandishi wa habari mkongwe
Kyaloeichi Oko Kessy (62) amefariki usiku wa kuamkia jana nyumbani kwake Pugu
jijini Dar es Salaam.
Mpwa wa marehemu Tumaini Msengi
alisema leo kuwa marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kisukari na
shinikizo la damu kwa muda mrefu na amekuwa akitibiwa katika hospitali
mbalimbali za jijini Dar es Salaam hadi jana ambapo mauti yalimkuta.
Kabla hajaanza kuugua Kessy alikuwa
mwandishi wa kujitegemea akiandika zaidi uchambuzi na makala katika vyombo mbalimbali
vya habari nchini yakiwemo magazeti ya Motomoto,Shaba,Rai, na mengineyo mengi
pia alikuwa ni mtunzi wa vitabu vya aina mbalimbali.
Msengi ameeleza kuwa marehemu ameacha watoto wawili na mipango ya
mazishi inafanyika nyumbani kwa mdogo wake Chanika nje kidogo ya jiji na
mazishi yanatarajiwa kufanyika wiki ijayo.
Marehemu ni mzaliwa wa kijiji cha
Rosho Kilema mkoani Kilimanjaro.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa, Jina la Bwana lihimidiwe.
Mawasiliano zaidi
0 comments:
Post a Comment