Kulia
Mkurugenzi wa TAHA Bi. Jacqueline Mkindi akiwa na Mgeni rasmi ndugu
Athumani Karunde wakati wa kutembelea mabanda ya waoneshaji
Mgeni
rasmi akipata taarifa za namna TAHA inavyofanya kazi ya kuwahudumia
wakulima na kuwaunganisha na fursa za mikopo ya kilimo biashara kutoka
kwa maofisa wa TAHA
Wakulima wakipokea maelezo ya namna ya kuunganishwa na fursa za Mikopo toka kwa maafisa wa TAHA
Asasi
zisizo za kiserikali zinazojishughulisha na shughuli za Kilimobiashara
za masharika ya TAHA, SNV,MVIWATA, AGRO PRO FOCUS,HIVOS, TCCIA na TRIAS
leo zimefanikisha kufanya maonesho ya Kuunganisha Wakulima na Fursa za
Mikopo ambayo yamelenga kuwakutanisha wakulima na wafanya biashara wa
mazao ya kilimo pamoja na Taasisi za kifedha na zile zinazotoa mikopo
kwa ajili ya shughuli za Kilimo Biashara katika picha ni Eneo
la viwanja vya Kwaraa Halmashauri ya Wilaya ya Babati ambavyo
vinatumika kwa kwa ajili ya kuwakutanisha wakulima na taasisi za kifedha
zinazotoa mikopo kwa wakulima(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
Afisa wa NMB akifafanua jambo kwa mkulima wakati wa maonesho hayo
yaliyofanyika Katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati kwenye Viwanja vya
Kwaraa na yamefunguliwa na Mwenyekiti wa chemba ya biashara Mkoa wa
Manyara ndugu Athumani Karunde.
Eneo la maonesho
Wakulima wakifuatilia hotuba na semina elekezi za wataalamu wa masuala ya biashara
Tom Olesika, Mkurugenzi wa Agri Pro Focus akinena jambo wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo
0 comments:
Post a Comment