MGOMO wa madereva wa mabasi yaendayo
mikoani na daladala zifanyazo safari za ndani katika mikoa mbalimbali nchini
Tanzania ulimalizika juzi baada ya kudumu kwa saa 31.
Mgomo huu ulimalizika kutokana na
ushawishi wa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda aliyezungumza na madereva hao kupitia viongozi wao wa Chama cha
Madereva Tanzania (CHAMAMATA) ambapo
walikubaliana mambo kadhaa ambayo walikuwa wakiyalalamikia.
Hii haikuwa mara ya kwanza kwa
madereva hao kugoma huku kimsingi wakiwa na hoja madhubuti za kudai maslahi yao
kutoka kwa waajiri wao ambao ni wamiliki wa mabasi hayo.
Awali itakumbukwa kuwa mgomo kama
huo ulifanyika Aprili 10 nchini kote na kuamua kuurejea tena baada ya kuona kiliochao
hakija tekelezwa.
Binafsi nilifarijika kuona huduma za
usafiri wa mabasi ya mikoani na daladala, zilizokuwa zimekwama kwa saa 31 ukirejea
katika hali yake ya kawaida.
Hii nikutokana na kwamba wapo
wagonjwa waliohitajika kusafiri kwenda kupata huduma mahospitalini na wanafunzi
waliokuwa wakifanya mitihani ya kuidato cha sita kuchelewa katika vyumba vyao
vya madarasa.
Viongozi wa ina ya Makonda
wanahitajika katika maeneo mengi nchini ili kuweza kutumia hekima na busara
katika ufumbuzi wa mambo na migogoro inayoibuka katika jamii kama hii na hata
ile ya ardhi kabla ya viongozi wa juu kufuka.
Madereva wale awali walimhitaji
Waziri Mkuu Mizengo panda kufika mahala pale na kuzungumza nao juu ya hatma yao
lakini kumbe Makonda alitosha; Safi sana.
Lakini baada ya kumaliozika kwa
mgomo wa awali, tulishuhudia ajali nyingi sana zilizopoteza maisha ya
watanzania wengi wakiwepo baadhi ya madereva wa mabasi hayo.
Chonde chonde ndugu zangu madereva
hebu awamu hii msituletee vilio na majonzi katika jamii zetu kwa ajali ambazo
nyingine zinaweza kuepukika kwa busara na hekima zenu za barabarani.
Ingawaje tayari juzi baada ya kuanza
safari majira ya mchana tulipata habari ya ajali ya basi huko mkoani Mbeya
lakini nawasihi na Mungu awasaidie zisiendelee tena kutokea.
Mkazingatie sheria za usalama
barabarani lakini pia busara zenu zinahitajika, kwani inawezekana kabisa alama
ya barabarani inakutaka utembee spidi 80 lakini mvua kubwa inanyeshabasi
punguza mwendo na uende ambao hautaleta athari kwako na abiria uliowabeba
pamoja na mali.
Nae Mwenyekiti wa Umoja wa Madereva
nchini, Clement Masanja, pia aliwataka madereva kuanza safari kwa kufuata
sheria za barabarani kwa kuwa mwisho wa haki zao unafuatiliwa.
Masanja alisisitiza sana tahadhari
barabarani, kwani kufika salama huko waendako ni moja ya sifa bora za dereva
mzuri.
Abiria na sisi pia hatuna budi kuwa
watulivu na kuacha tabia za kuwasema vibaya madereva wawapo safarini kuwa
mabasi yao hayakimbii na matokeo yake ni kusababisha ajali.
Tuepuke ushawishi mbaya wa mwendo
kasi kwani daima safari ni hatua na polepole ndio mwendo na wahenga wanasema
“Kawia Ufike.”
Porojo hii ilichapishwa leo kwa mara ya kwanza katika gazeti la Habarileo kama WAZO.
0 comments:
Post a Comment