Meneja
wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi akionyesha
sehemu ya vitabu kabla ya kukabidhi msaada wa vitabu vya masomo ya
sayansi vyenye thamani ya milioni 4/-, kupitia Mradi wa ‘Airtel Shule
Yetu’ kwa Shule ya Sekondari ya King’ongo iliyopo Kimara katika Manispaa
ya Kinondoni jijini Dar es Salaam jana. Waliokaa (kutoka kushoto) ni
Meneja wa Airtel Tawi la Kinondoni, Fadhili Mwasyeba, Mwenyekiti wa Bodi
ya Shule hiyo, Godfrey Mheluka na Mkuu wa Shule hiyo, Nyaibuli Bhoke.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Shule ya Sekondari ya King’ongo, Godfrey Mheluka (kulia),
akikabidhi msaada wa vitabu vya masomo ya sayansi vyenye thamani ya
milioni 4/-, kwa Mkuu wa Shule hiyo, Nyaibuli Bhoke baada ya kukabidhiwa
na Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi
(kushoto), kupitia Mradi wa ‘Airtel Shule Yetu’ katika hafla
iliyofanyika shuleni hapo Kimara jijini Dar es Salaam jana.
Meneja
wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (wa pili
kushoto), akikabidhi vitabu vya masomo ya sayansi vyenye thamani ya
milioni 4/-, kupitia Mradi wa ‘Airtel Shule Yetu’ kwa baadhi ya
wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya King’ongo, katika hafla iliyofanyika
shuleni hapo Kimara jijini Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia (kutoka wa
pili kushoto)ni Mwenyekiti wa Bodi ya shule hiyo, Godfrey Mheluka, Afisa
Elimu na Takwimu wa Manispaa ya Kinondoni, Omary Ahmed na Mkuu wa Shule
hiyo, Nyaibuli Bhoke .
Wanafunzi
wa Shule ya Sekondari ya King’ongo wakifurahia vitabu vya masomo ya
sayansi, baada ya Kampuni ya Airtel kupitia Mradi wake wa ‘Airtel Shule
Yetu’ kukabidhi vitabu vyenye thamani ya milioni 4/- kwa shule hiyo
katika hafla iliyofanyika shuleni hapo Kimara jijini Dar es Salaam jana.
0 comments:
Post a Comment