Mojawapo ya ndiga zilizoshindaniwa likioneshwa
Mkuu
wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Said Meck Sadik akiongea na Dennis Ssebo
wa 97.3 EFM kwenye hafla hiyo jana katika uwanja wa Tanganyika Packers,
Kawe. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mhe. Paul Makonda
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Said Meck Sadik akimkabidhi ndinga yake mshindi Stella Joseph kutoka wilaya ya Ilala
Mkuu
wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Said Meck Sadik akimpongeza mshindi
Gabriel Robert kutoka wilaya ya Temeke bada ya kumkabidhi ndinga
Mojawapo ya ndiga zilizoshindaniwa
*******
Hatimaye
Washindi wa shindano la Shika Ndinga la 93.7 EFM wamepatikana baada
ya mchuano mkali uliofanyika jana Aprili 25, 2015 katika viwanja vya
Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es salaam.
Fainali
hiyo iliwahusisha washiriki 10 kutoka katika wilaya zote tatu za mkoa
wa Dar-es-salaam watano kati yao wakiwa wanawake watano wakiwa ni
wanaume.
Shindano
hilo lilihudhuriwa na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Said Meck
Sadik akiwa kama mgeni rasmi, Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mhe. Paul
Makonda na Mstahiki Naibu Meya wa wilaya ya Temeke Mhe. Juma mkenga. Mhe
Sadik alisema ni ubunifu wa hali ya juu ulioneshwa na kituo cha 93.7
EFM kwa kuanzisha shindano la aina yake ambalo litaongeza ajira kwa
vijana na kuinua hali zao za uchumi.
Mkuu
wa Mkoa huyo pia aliwaasa washindi kutumia ndinga walizoshinda ili
kujiendeleza kiuchumi.
Kwa upande wake Mhe. Paul Makonda alisema vijana wajifunze kujitokeza
katika mashindano kama haya maana zaidi ya kuburudisha yanabadilisha
maisha yao kwa namna yatofauti.
Washindi
waliojishindia ndinga kwa upande wa wanaume ni Gabriel Robert kutoka
wilaya ya Temeke mwenye umri wa miaka 36 na Stella Joseph kutoka wilaya
ya Ilala mwenye umri wa miak 26 ambao kwa pamoja wamesema shindano
halikuwa rahisi na wanafuraha kubwa ya kujishindia gari hizo ambazo
watazitumia katika biashara zao.
Aidha
wameishukuru redio ya 93.7 EFM kwa kuandaa shindano hilo na kuwashauri
wasikilizaji waendelee kusikiliza redio hiyo maana inajali wasikilizaji
wake.
0 comments:
Post a Comment