Balozi Liberata Mulamula, Balozi wa Tanzania nchini Marekani akifungua mkutano wa Mabalozi wa Heshima uliofanyika siku ya Ijumaa April 24, 2015 Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani. Mkutano huo ulizungumzia uwekezaji na Utalii zikiwemo Changamoto zake na jinsi ya kukabiliana nazo. Pia katika mkutano huo uliokua sehemu ya maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano uliudhuria pia na Viongozi wa Taasisi za Diaspora wa Tanzania ambao wanaguswa na kuiona nchi yao ikipiga hatua ya maendeleo katia sekta ya uwekezaji na Utalii.
Abdul Majid mwanaDiaspora Mtanzania anayeishi California nchini Marekani akielezea huduma kwa wateja bado ipo kiwango cha chini nchini Tanzania na jinsi gani ikiboreshwa inavyoweza kunua uchumi wa Tanzania.
Balozi wa Heshima Mhe. Kjell Berch akichangia na kuelezea majukumu ya Balozi wa heshima.
Rais wa East Africa Diaspora Business Counsil Benedict Kazora ambaye pia ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Dallas, Texas akichanganua na kutoa maelezo yanayoweza na kurahisiha maswala ya uwekezaji na kukosoa baadhi ya makampuni yanavyowekeza Afrika kwa kujinufaisha yenyewe.
Karen Hoffman Rais wa The Bradford Group kutoka New York akielezea sekta ya Utalii na utangazaji wa Utalii wa Tanzania nchini Marekani.
Balozi wa Heshima Mhe.Cemil Teber kutoka New Mexico akichangia jambo.
Balozi wa Heshima kutoka Ohio Mhe. Patrick Griswold akielezea sekta ya uwekezaji na changamoto inazokutana nazo huku akitoa mfano wake mwenyewe alipokua meneja mkuu wa General Tire miaka ya nyuma na tangia alipoondoka kiwanda kikafa na sasa anatarajiwa kwenda tena Tanzania kujaribu kukifufua upya kiwanda hicho.
Mkutano wa Balozi Liberata Mulamula na Mabalozi wa Heshima ukiendelea
Wakati wa chakula. Picha zote na Vijimambo, Kwanza Production
0 comments:
Post a Comment