Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akipunga
mkono kuwasalimia wananchi wakati alipokuwa akiwasili kwenye Uwanja wa Uhuru,
Jijini Dar es salaam, leo kwa ajili ya kuhudhuria Sherehe za Maadhimisho ya
Miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Kushoto ni Mkuu wa Majeshi ya
Ulinzi na Usalama, Davis Mwamunyange
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akiwa na baadhi ya Viongozi wenzake wa Serikali, wakisimama kutoa
heshima wakati ikipigwa mizinga 21, uwanjani hapo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akikagua
gwaride la heshima, wakati wa sherehe za Maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es
Salaam, leo.
0 comments:
Post a Comment