Ilikua mishale ya saa kumi kamili jioni ujumbe wa
harakati za Imetosha ulipowasili katika kituo cha Buhangija cha
kulea watoto wenye mahitaji maalumu mjini Shinyanga. Sauti za furaha
za watoto zilisikika zikiimba nyimbo za kukaribisha ujumbe wa wana harakati hao
ambao wako Mwanza kutambulisha harakati za Imetosha ambazo ni kupambana na kupinga unyanyapaa, ukatili na mauaji kwa watu wenye Ulemavu wa ngozi.
wajumbe wa Imetosha wakiongea na watoto kituoni hapo Mwenyekiti wa harakati za
Imetosha Masoud Ali (Kipanya) alisema Imetosha inatambua umuhimu wa haki ya kuishi kwa
kila binadamu ndio maana Imetosha imeanzisha harakati za kutokomeza mauaji na
unyanyapaa kwa watu wenye ulemavu wa ngozi. “Tunatambua hapa kati yenu kuna vipaji vya aina
mbalimbali hivyo pamoja na kupambana na harakati za kupinga na kutokomeza
mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi tupo hapa kuwatia moyo kuwa mna uwezo
mkubwa ndani yenu hivyo msijidharau” alisema Masoud.
Balozi wa Imetosha Henry Mdimu akinunua mahitaji ya watoto waliopo kituoni hapo kabla ya kufika kituoni hapo.
Katibu wa Imetosha amabaye ki taaluma ni mwandishi wa habari akimhoji mwalimu Francis Ajali.
PICHA ZAIDI BOFYA>>>> KIDEVU MATUKIO
0 comments:
Post a Comment