Mwakilishi
wa Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB, Winfrida Igogo akitoa mada katika
mafunzo ya wanafunzi wanaosoma masomo ya manunuzi na ugavi katika Chuo
cha TIA Mbeya.
Wanafunzi
ambao wanasoma masomo ya manunuzi na ugavi wakifuatilia mafunzo
yaliyotolewa na Bodi ya manunuzi na ugavi katika chuo cha uhasibu Mbeya.
***************
BODI
ya manunuzi na ugavi (PSPTB) imetoa mafunzo kwa wanafunzi waosoma
masomo ya manunuzi na ugavi katika chuo cha uhasibu(TIA) Mbeya.
Katika
mafunzo hayo wito ulitolewa kwa Taasisi binafsi na serikali kuepuka
kutoa ajira katika sekta ya manunuzi na ugavi kwa watu ambao hawana
taaluma hiyo wala kusajiliwa na Bodi ya PSPTB.
Wito
huo ulitolewa na Mwakilishi wa Mkurugenzi mtendaji wa Bodi ya Manunuzi
na ugavi(PSPTB), Winfrida Igogo, alipokuwa akijibu maswali kutoka kwa
Wanafunzi wa taasisi ya Uhasibu kampasi ya Mbeya ambao ni wanachama wa
Umoja wa wanataaluma wa manunuzi na Ugavi(PSA-TIA) wakati wa mafunzo
yaliyofanyika katika ukumbi wa TIA Mbeya.
Igogo
alisema hairuhusiwi kwa mtu yoyote kufanya kazi za manunuzi na ugavi
bila kuwa na utalaam pamoja na kusajiriwa na bodi kwani kufanya hivyo ni
kosa kisheria jambo ambalo adhabu inamkumba pia mwajiri.
Alisema
lengo la kutoa mafunzo kwa wanafunzi wanaosoma masomo ya manunuzi na
ugavi(procurement & supply)ni kuwajengea uwezo na kuwahamasisha juu
ya taratibu wanazopaswa kuzifuata wakiwa kazini kuhusiana na manunuzi na
ugavi.
Aliongeza
kuwa lengo lingine ni kuwakumbusha wanataaluma hao kujisajili na bodi
mara baada ya kuhitimu masomo yao jambo ambalo litasaidia upatikanaji wa
ajira haraka tofauti na wasio sajiliwa ambao hukaa muda mrefu bila
ajira kutokana na kukosa kipengere cha uzoefu.
Alisema
Bodi ipo kwa mujibu wa sheria ambapo hivi sasa ipo kwenye mchakato wa
kupitia kila taasisi kukagua kama walioajiriwa wanasifa za manunuzi na
ugavi ikiwa pia kupitia matangazo mbali mbali ya ajira kama vigezo
vinavyowekwa vipo kwa mujibu wa sheria.
Kwa
upande wake Mwezeshaji mwingine katika mafunzo hayo, Juvenal Joseph,
alisema ni vema wataalamu wa manunuzi na ugavi wakazingatia sheria kwa
kuepuka mikataba inayoweza kuwaingiza matatizoni.
Alisema
wataalam wa manunuzi na ugavi wanapaswa kujua kuwa kila mikataba ni
makubaliano lakini sio kila makubaliano yanaweza kuwa mikataba hivyo
wajiepushe kutumbukia katika rushwa kwa kukiuka taratibu za manunuzi na
ugavi.
Naye
Mlezi wa Wanafunzi wa Taasisi ya Uhasibu (TIA) Kampasi ya Mbeya
aliyejitambulisha kwa jina moja la Mgaya alisema Wanafunzi wanaosomea
masomo ya manunuzi na ugavi wanapaswa kuwa na nidhamu katika masomo yao
ili kuepuka kuwa maafisa wav yeti.
Aidha
Mwalimu wa Somo la Manunuzi na ugavi chuoni hapo, aliyejitambulisha kwa
jina la Gasibila aliishukuru bodi kwa kuendesha mafunzo hayo na
kuongeza kuwa jambo hilo litasaidia kuzalisha wahitimu wenye taaluma na
kupata watumishi waliotukuka.
Aliongeza
kuwa waalimu na watumishi katika fani ya manunuzi na ugavi wanategemea
maelekezo kutoka miongozo kutoka bodi kwa kuwa wao ndiyo dira ya
utumishi mzuri nchini.
0 comments:
Post a Comment