Na Father Kidevu Blog, Morogoro.
WATU 18 wamepoteza maisha papo hapo kwa kuteketea na moto huku wengine 11
wakijeruhiwa vibaya kwa moto kufuatia magari mawili kugongana ambayo ni
Basi Scania mali ya kampuni ya Nganga lililosajiliwa kwa namba T373 DAH na gari ;la mizigo Mistubishi Fuso T164 BKG.
Ajali hiyo imeelezwa kutokea majira ya asubuhi saa mbili katika
Kijiji cha cha Msimba, Tarafa ya Mikumi, Wilayani Kilosa mkoani Morogoro.
Polisi mkoani Morogoro kupitia kwa Kamanda wake, Leonald Paulo imesema
chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa Basi la Nganga kuendesha gari kwa mwendo
kasi na kulipita gari lillilo mbele yake bila kuchukua tahadhari na kusababisha
ajali hiyo.
Kamanda Paulo aksema basi lilikuwa limepakia pikipiki katika
buti na ambayo ilikuwa na mafuta hivyo baada ya kugongana palitokea mlipuko na
kusababisha moto mkubwa ulioteketeza basin a lori hilo.
Mbali na abiria waliokufa ni madereva wa magari yote mawili
walioteketea kabisa na moto huo na abiria walioshindwa kujiokoa na majeruhi
takribani 11 walikimbizwa katika Hospitali ya Mtakatifu Kizzito Mikumi.
Father Kidevu Blog inatoa pole kwa wote waliopoteza ndugu na kwa majeruhi na abiria wote.
0 comments:
Post a Comment