Mteja wa muda mrefu wa bidhaa zinazouzwa kwenye maduka ya Woolworths ambaye pia alikuwa Mgeni rasmi Manfred Ngantunga (katikati) akikabidhiwa zawadi na mfanyakazi wa duka hilo, baada ya kuzindua punguzo la bei la bidhaa kwa asilimia 50%zinazouzwa kwenye maduka ya hayo Tanzania, Kulia ni Meneja Mkuu wa Woolworths Joehans Bushiri,Hafla ya uzinduzi ilifanyika makao makuu ya woolworths jijini Dar es Salaam.
Mteja wa muda mrefu wa bidhaa zinazouzwa kwenye maduka ya Woolworths ambaye pia alikuwa Mgeni rasmi Manfred Ngantunga (katikati) akikabidhiwa zawadi na mfanyakazi wa duka hilo, baada ya kuzindua punguzo la bei la bidhaa kwa asilimia 50%zinazouzwa kwenye maduka ya hayo Tanzania, Kulia ni Meneja Mkuu wa Woolworths Joehans Bushiri,Hafla ya uzinduzi ilifanyika makao makuu ya woolworths jijini Dar es Salaam.
**********
Na Mwandishi Wetu
Katika
pindi hiki cha sikuu ya Pasaka watanzania wanaweza kununua nguo zenye
ubora kwa nusu bei kufuatia punguzo la silimi 50 lililotangazwa jana na
duka maarufu la nguo la Woolworths jijnini Dar Es Salaam.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa punguzo hilo, mkurugenzi wa duka hilo Joehans
Bushiri aliawambia wateja waliofika dukani hapo kuwa punguzo hilo
titadumu kwa muda wa wiki nne.
Alisema lengo kubwa la Woolworths ni kuwawezesha watanzania wenye vipato vya aina mbali mbali kufurahia sikukuu ya Pasaka kwa kupata nguo za kisasa zenye ubora kwa gharama nafuu.
Mkurugenzi
huyo pia aliwaasa watanzania kuachana na nguo za mtumba“Tunawasihi
watanzania kuepukana na matumizi ya nguo za mtumba kwani si salama kwa
afya zao. Katika kipindi hiki cha sikukuu ya Pasaka duka la Woolworths
linatoa punguzo kubwa ili kuwawezesha watanzania kupata nguo mpya na
zenye ubora.,” alisema.
Bushiri
alisema duka hilo ambalo ni moja kati ya maduka makubwa ya nguo hapa
nchini, litaendelea kuwahudumia wateja wake kwa kuwaletea nguo nzuri na
zenye ubora kwa gharama nafuu na hivyo kuwasaidia kuepukana na nguo za
mtumba.
“Mteja
anayekuja kununua nguo dukani kwetu anakuwa amefanya uamuzi sahini
kwani atapa nguo zenye ubora kwa gharama nafuu na atakuwa amepata kitu
ambacho kinaendana na thamani ya pesa yake,” alieleza
Mkurugenzi
huyo aliongeza kuwa, duka hilo pia linatoa nafasi kwa wateja kununua
nguo kwa kulipia kidogo hadi kwa muda wa miezi mitatu ili kuwawezesha
wale wasio na fedha za kutusha kulipa mara moja kuweza kufurahia nguo
zenye ubora.
Kuhakikisha
wateja wetu wanapata vitu bora kabisa, vinavyoendana na wakati na kwa
mda muafaka, Woolworths imeweza kubadilisha mfumo wa uletaji wa bidhaa
nchini badala ya kutumia meli kama zamani sasa inatumia usafiri wa
ndege. Kabla ya hapo tulikuwa tun kunatumia muda wa mwezi mmoja hadi
miwili kufikisha mizigo nchini wakati kwa sasa tunatumia mda wa wiki
mbili hadi tatu.
Bwana
Bushiri pia akasisitiza kwamba anapenda kuwahakikishia wateja wao
kwamba Woolworths Tanzania ina bidhaa zote kama zinazopatikana South
Africa na kwa bei zinazofaa kabisa.
Kwa
upande wake Manfred Ngatunga ambaye ni mmoja kati ya wateja wazuri wa
duka hilo alitoa shukrani zake kwa uongozi wa duka hilo kwa kutoa
punguzo kubwa haswa katika mismu huu wa sikuu ya Pasaka.
Uamuzi
wa punguzo la bei umekuja kipindi kizuri sana. Kipindi hiki na kipindi
ambacho familia zinafanya manunuzi kwa ajili ya sikuu ya Pasaka.
Tunashukuru kwa kuwa tutapata nguo zenye ubora kwa nusu bei, kila mtu
sasa anaweza kupendeza,” alieleza.
0 comments:
Post a Comment