Meneja Mkuu wa Mgodi wa North Mara, Gary Chapman, akionyesha wafanyakazi wenzake wa mgodi huo, tuzo ya umahiri ya mwaka 2014, (Excellence Awards 2014), waliyonyakua kwa kuwa mgodi wenye kuzingatia usalama kwa kiwango cha juu, wakati wa utoaji tuzo hizo awamu ya pili iliyofganyika kwenye mgodi huo Jumanne usiku Machi 23, 2015.
Meneja mkuu wa mgodi wa North Mara, Gary Chapman, (kushoto), akishuhudia wakati Le Poer Trench, (katikati) na Albert Rudman, wakionyesha tuzo za umahiri za mwaka 2014, ( ECellence Aawards 2014), walizopokea kwa niaba ya idara ya huduma za kiufundi ya mgodi huo, kwenye hafla ya awamu ya pili ya utoaji tuzo hizo iliyofanyika kwenye mgodi huo ulioko Nyamongo wilayani Tarime mkoa wa Mara, Jumanne usiku Machi 23, 2015
Meneja Mkuu wa Mgodi wa North Mara, Gary Chapman, (kushoto),
akimkabidhi Aziz Rashid, kwa niaba ya idara anayofanyia kazi ya Matengenezo, tuzo ya umahiri ya mwaka 2014, itolewayo na kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia, kwenye hafla ya awamu ya pili ya utoaji tuzo hizo iliyofanyika kwenye mgodi huo wilayani Tarime mkoa wa Mara Jumatatu usiku Machi 23, 2015. Tuzo hizo utolewa kila mwaka kwa mfanyakazi binafsi au idara, kutokana na umahiri katika kutekeleza majukumu yao kwa weledi na nidhamu ya hali ya juu.
Meneja wa uchimbaji wa mgodi wa dhahabu North Mara, Jimmy Ijumba, (kushoto), akimpa tuzo ya umahiri, mfanyakazi wa kitengo cha usalama cha mgodi huo, Kashaka Goda, wakatiwa utoaji tuzo za umahiri mwaka 2014 awamu ya pili zilizofanyika kwenye mgodi huo, huko Nyamongo, wilayani Tarime mkoa wa Mara juzi Jumanne. Tuzo hizo hutolewa kila mwaka na kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia, inayomiliki migodi mitatu ya Bulyanhulu, North Mara na Buzwagi.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa North Mara, Gary Chapman, (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa idara ya matenegenezo ya mgodi huo, baada ya kuwapatia tuzo na vyeti kwenye hafla ya awamu ya pili ya utoaji tuzo za umahiori mwaka 2014, zilizofanyika kwenye mgodi huo Jumanne usiku Machi 23, 205. Tuzo hizo utolewa kila mwaka kwa mfanyakazi binafsi au idara, kutokana na umahiri katika kutekeleza majukumu yao kwa weledi na nidhamu ya hali ya juu.
0 comments:
Post a Comment