MCHEZAJI wa zamani wa Simba na Timu ya Taifa ya
Tanzania “Taifa Stars”, Dua Said na muingizaji wa Bongo Movie, Lumole Matovola “Big”
na Mwenyekiti wa Wasanii Tanzania (SHIWATA),
Cassim Taalib ni miongoni mwa wasanii 48 walioamua kwenda kuanza maisha ya
kijijini.
Wakizungumza katika mkutano wa bodi ya SHIWATA jana,
wasanii hao walisema meamua kuungana na wasanii wengine wanaokwenda kuanza
maisha mapya katika kijiji cha Wasanii, Mwanzega Mkuranga ambapo watapatiwa
mashamba ya kulima bustani na mazao ya muda mfupi.
Dua Said alisema amevutika na kujiji hicho na
amekuwa mmoja wa wachezaji wa zamani kuanza maisha ya kijiji cgha wasanii
ambayo alisema ni mazuri yenye manufaa kulinganisha na maisha ya mjini.
“Nimefika kijijini Mwanzega na mimi nimejengewa
nyumba yangu na SHIWATA, pia nimerekodi filamu ambayo mtaiona katika luninga ni
maisha mazuri ya kijijini ambayo huwezi
kufananisha na mjini” alisema Big.
Mwenyekiti
wa SHIWATA, Taalib alisema kati ya wanachama 8,000 ambao wamepanga kuhamia Mkuranga
kwa ajili ya kilimo na ufugaji watashiriki katika sherehe za kutimiza miaka
kumi kutoka ianzishwe na jumla ya nyumba 134 zimejengwa.
Alisema
mtandao huo unasikitishwa na taarifa ambazo siyo za kweli kuwa ndani ya mtandao
huo kuna utapeli na kuongeza kuwa wanataarifu wanachama wo wote kwamba mpango huo
ni wa kweli, uhakika na uwazi hakuna mwanachama hata mmoja atakayepoteza
haki yake kwa kujiunga na SHIWATA.
Alisema Wanachama waliojiunga na SHIWATA kutoka mwaka 2004 na kufanikiwa kulipa sh. 10,000 za kujiunga na kijiji cha Mwanzega kupitia mtandao huo na kupatiwa hati wanatakiwa kufika ofisini Ilala Bungoni na nyaraka zao zote ili wapelekwe kijijini kukabidhiwa maeneo yao.
Alisema pia wanachama wote waliochangia ujenzi ya nyumba zao kwa kiasi chochote cha fedha kupitia benki wanatakiwa kufika ofisini na nyaraka zao zote ili nao wakakabidhiwe maeneo yao kwa kadri walivyochangia.
Alisema waliochangia katika mgawo wa mashamba katika shamba la Ngarambe na hatajakabidhiwa mashamba yao wanatakiwa wafike ofisini na nyaraka zao ili wakakabidhiwe.
Alisema kijiji ambacho wanaamini kitakuwa kivutio kwa watalii nchini kitapewa jina la Tallywood na kutangazwa nchi mbalimbali duniani na kitakuwa maarufu kwa utengenezaji filamu ambazo zitauzwa ndani na nje ya Tanzania.

0 comments:
Post a Comment