Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Arusha,Isaack Joseph akizungumza
na waandishi wa habari leo katika makao makuu ya chama hicho na kudai
kushangazwa na kauli ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa,Nape
Nnauye ya kuwa makundi yanayokwenda nyumbani kwa Mbunge wa Monduli na
Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowasa,kumshawishi kugombea Urais kuwa na
kusema kuwa makundi hayo ynachokifanya ni utekelezaji wa kauli ya
Mwenyekiti wa CCm Taifa Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa katika sherehe za
CCM mjini Songea, alipowaruhusu watu wakawashawishi wanaoona wanafaa
kuwania nafasi mbalimbali.(Source: http://jamiiblog.co.tz/
Mwenyekiti
wa Umoja wa Vijana wa CCM(UVCCM),Mkoa wa Arusha,Robinson
Meitinyiku,akizungumza katika mkutano huo na waandishi wa Habari,ambapo
amekitaka Chama hicho kusimamia misingi,katiba na kanuni kwa wanachama
na kukaripia wote wanaofanya makosa na kumtaka Nape kuheshimu na
kutambua maadili ya utu na kumtaka atambue kuwa Lowasa ana watu nyuma
yake ambao wanampenda,kumheshimu na kumjali,hivyo UVCCM hawatakaa kimya
kuwasemea wanyonge wanaokwenda kumshawishi Lowasa agombee..hapo
akifafanua Katiba ya CCM inavyowapa wanachama fursa ya kuwaona viongozi
wao.
Katibu Mwenezi akizungumza na waandishi wa habari leo,katika Makao Makuu ya Chama hicho.
Kulia
ni Mwandishi wa habari wa Kituo cha Radio5,Arusha Mohamed na kushoto ni
Grace Macha wa Tanzania Daima,wakifuatilia mkutano huo.
**********
Na Pamela Mollel,Arusha
Chama
Cha Mapinduzi(CCM)mkoa wa Arusha kimesema hakipingani na makundi
yoyote yanayokwenda kumshawishi Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu
Mstaafu,Edward Lowasa kuchukua fomu ya kuwania urais katika uchaguzi
Mkuu unaotarajiwa kufanyika Mwezi Oktoba mwaka huu na kusema kuwa Sauti
ya watu ni Sauti ya Mungu.
Aidha Umoja wa Vijana wa CCM(Uvccm) mkoani hapa kimedai kushangazwa na kauli
ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM,Nape Nnauye,ya kudai kuwa kitendo
cha makundi ya watu wanaokwenda nyumbani kwa Lowasa kumshawishi agombee
Urasi, hakumwondolei Lowasa sifa za kuwania urais kwa kuwa hakuna
kipengele kwenye Katiba au Kanuni ya CCM kinachokataza wanacahama kufata
viongozi.
Hayo yalisemwa jana jijini hapa na Katibu
wa itikadi na uenezi wa CCM mkoani hapa,Isaack Joseph alipokwua
akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya chama hicho na
kusema kuwa kimeshangazwa na kauli ya Nnauye kwani kinachofanyika ni
utekelezaji wa kauli ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa katika sherehe za
CCM mjini Songea alipowaruhusu watu wakawashawishi wanaoona wanafaa
kuwania urais.
Alisema
kwamba kwa tabia na mila za kiafrika mtu akitembelewa na mgeni hana
budi kumkaribisha ,kumkirimu pamoja na kumfanyia maandalizi yote na
kusema kuwa makundi mbalimbali yameona Lowasa anafaa ndio maana
yamekwenda kumshawishi agombee.
“Kama
kuna makundi yanayomfuata Lowasa na yaende kwani Sauti ya watu ndio
sauti ya Mungu watu wameona anafaa ndio maana wamemfuata kumshawishi
sasa kunamuondoleaje sifa?”alihoji Joseph
Hatahivyo,alisema
kuwa Lowasa tangu apewe adhabu ndani ya chama hicho hakuwahi kuongea
lolote na hata baada ya kufunguliwa adhabu hiyo baadhi ya makundi
yamekuwa yakimfuata kwa kuona anafaa na kumtaka Nnauye kuacha kuropoka
hovyo.
Kwa upande
mwenyekiti wa Uvccm mkoani Arusha,Robinson Meitinyiku alimshangaa Nnauye
kwa kauli yake kwa kuwa katiba ya chama hicho ibara ya 14 inamruhusu
mwanachama yoyote kumtembelea kiongozi wake kwa kufuata taratibu.
Alisema
kuwa kuna baadhi ya makundi ambayo yamekuwa yakiwashawishi baadhi ya
makada wa CCM na hata wengine kutoa sadaka na vitabu kuwanadi wagombea
wao lakini hawakemewi zaidi ya Lowasa,jambo linaloonyesha Nape kuegemea
upande mmoja.
Alimtahadharisha
Nnauye kwamba Lowasa ni kiongozi mkubwa hapa nchini na ana wafuasi
wengi nyuma yake hivyo hata wao wakiona anafaa kugombea Urais na
wakipata fursa ya wkenda kumtembelea na kumshawishi wataenda.
“Lowasa
ana watu wengi nyuma yake tunamheshimu na sisi kama vijana wa Arusha
tuna haki zote kumtetea tutamfuata hivi karibuni kumshawishi agombee
hatuwezi kukaa kimya kwa kuwa tunaona anafaa”alisema Meitinyiku.
0 comments:
Post a Comment