Waziri wa
Nishati na Madini, George Simbachawene (kulia) akipokea Tuzo ya Kimataifa
ya mwaka ya Maendeleo ya Udhibiti wa Sekta ndogo ya Mafuta na Gesi inayotolewa
na Kampuni ya Kimataifa ya Wildcat International, ya nchini Marekani kupitia machapisho
yake maarufu Duniani ya The Oil & Gas Year (TO&GY). Anayemkabidhi Tuzo
hiyo ni Mratibu wa Mahusiano kwa Wateja kutoka Jarida la TO&GY, Bi. Laura
Carr.
***********
Wizara ya
Nishati na Madini imepata Tuzo ya Kimataifa ya mwaka ya Maendeleo ya Udhibiti
wa Sekta ndogo ya Mafuta na Gesi.
Tuzo hiyo ya mwaka 2014 inayotolewa
na Kampuni ya Kimataifa ya Wildcat International, ya nchini Marekani kupitia
machapisho yake maarufu Duniani ya The Oil & Gas Year (TO&GY), imekabidhiwa
rasmi jijini Dar es Salaam kwa Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene
ambaye alipokea Tuzo hiyo kwa niaba ya Wizara.
Tuzo hiyo, iliyotolewa na
Mratibu wa Mahusiano kwa Wateja kutoka Jarida la TO&GY, Bi. Laura Carr inaitambua
Wizara kutokana na mafanikio yake
katika kushughulikia changamoto za udhibiti wa sekta ndogo ya mafuta na gesi na
hivyo kuchochea maendeleo ya sekta hiyo.
Mafanikio hayo ni pamoja na
kuwa na sera mpya ya gesi asilia, kuwa
na muundo mpya wa makubaliano ya gharama za utafutaji na uzalishaji wa mafuta
na gesi (Production- Sharing Agreement), na kuwa na Rasimu ya Sera Uwezeshaji
na Ushirikishaji Wazawa (local content policy).
“Hayo ni baadhi tu ya maendeleo
yaliyofanya sekta hii kueleweka na kukubalika zaidi kwa wawekezaji na wadau,”
imesema sehemu ya Jarida la TO&GY.
Pamoja na Tuzo ya Wizara ya
T0&GY, Shirika la Umeme nchini kupitia Mkurugenzi wake, Mhandisi Felchesmi
Mramba ameshinda Tuzo ya Mtu wa Mwaka (Person of the Year, 2014) kutokana na mpango yake ya Dola za Kimarekani
Bilioni Sita zitakazowezesha TANESCO kuongeza uzalishaji umeme mara tatu zaidi
ya sasa kutokana na vyanzo mbalimbali
kama makaa ya mawe, gesi asilia na maji hivyo kuondokana na utegemezi wa
uzalishaji umeme kwa kutumia mafuta.
Aidha Shirika la Maendeleo ya
Petroli nchini (TPDC) limeshinda Tuzo ya transition
of the year (2014) kutokana na kupiga hatua katika shughuli zake ambapo
mbali ya kuwa kuwa mdhibiti wa sekta ndogo
ya mafuta na gesi bali pia limekuwa mwekezaji baada ya kushinda tenda na kupata
vitalu viwili kwa ajili ya utafiti wa mafuta na gesi nchini.
Usambazaji wa machapisho ya TO&GY
hukaguliwa na Taasisi ya Marekani ya BPA Worldwide inayokagua machapisho maalum
zaidi ya 2600 katika nchi 30 Duniani yakiwemo majarida maarufu ya Toronto Star,
Wall Street Journal na Gulf News.
0 comments:
Post a Comment