Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Maria Bilia akizungumza wakati wa
uzinduzi wa mafunzo ya wadadisi 200 wa Sensa ya Viwanda itayofanyika nchi
nzima mwezi huu. Mafunzo hayo yanafanyika chuo cha Takwimu Mashariki mwa
Afrika kilichopo eneo la Changanyikeni jijini Dar es salaam.
Mkuu wa chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika kilichopo eneo la
Changanyikeni jijini Dar es salaam Prof.Ngalinda Innocent akizungumza na
wadadisi watakaokusanya takwimu za Sensa ya Viwanda mwezi huu wakati wa
ufunguzi wa mafunzo ya siku 14.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa
akizungumza na wadadisi 200 watakaokusanya takwimu za viwanda wakati wa Sensa
ya Viwanda itakayofanyika nchini nzima mwezi huu leo eneo la Chuo cha Takwimu
cha Mashariki mwa Afrika jijini Dar es salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Shirikisho la wenye Viwanda nchini Bw.Hussein
Kamote akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wadadisi 200
watakaokusanya takwimu wakati wa Sensa ya viwanda itakayofanyika nchini
mwezi huu.
Baadhi ya wadadisi wa Sensa ya Viwanda wakifuatilia hafla ya
ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kukusanya takwimu sahihi wakati wa
Sensa ya Viwanda leo jijini Dar es salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Maria Bilia
akiwa katika picha ya pamoja na menejimenti ya NBS na wadadisi wa Sensa ya
Viwanda
0 comments:
Post a Comment