Nafasi Ya Matangazo

February 12, 2015



 Mwenyekiti wa Jumuia ya Vijana wa CUF Taifa (JUVICUF), Hamidu Bobali akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Februari 12,2015 kuhusian na maandamano yatakayo fanyika kesho licha ya kukosa kibali cha Jeshi la Polisi. Pamoja nae ni Mjumbe wa jumuia hiyo, Shani Beleko.
 Wanahabari wakichukua dondoo za mkutano huo.
Baadhi ya vijana ambao ni wanachama wa JUVICUF wakiwa katika mkutano huo.
************
CHAMA cha Wananchi  CUF kupitia Jumuiya ya Vijana wa Chama cha Wananchi (JUVICUF), kime[panga kufanya maandamano makubwa Februari 13, 2015 kuanzia Bugururuni Rosana hadi Ofisi za Tume ya taifa ya Uchaguzi na baade Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa JUVICUF, Hamidu Bobali amesema maandamano hayo yamenyimwa kibali na jeshi la Polisi lakini kwakuwa walisha jiandaa kuyafanya wao watayafanya ili kufikisha ujumbe wao .

“Tumeandaa manaandamano ya amani  kwa lengo la  kuitaka tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC),kuongeza siku za kuandikisha wapiga kura kutoka saba (7) zilizo pangwa sasa hadi 14 na kulaani  ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na polisi,” alisema Bobali.

Bobali Februari 9,mwaka huu waliliandikia jeshi la polisi barua ya  kuwataarifu juu ya kufanyika kwa maandamano hayo ya amani  na waliainisha maudhui ya maandamano hayo na kuwa ni kuitaka NEC,kuongeza siku za kuandikisha wapiga kura kutoka siku saba hadi 14, na kulaani ukiukwaji wa haki za binadamu  waliodai unafanywa na  jeshi hilo.

Majibu ya barua hiyo yaliyotolewa  leo na jeshi hilo, yamesitisha maandamano hayo kwa madai kuwa njia hiyo haiwezi kuleta suluhu la madai yao.

Maandamano hayo yamepamngwa kuanzia saa nne asubuhi.


Kufuatia sakata hilo, Kamishna wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova akizungumza na vyombo vya habari ofisi kwake ametangaza kupiga marufuku maandamano hayo kwa kile alichoeleza kuwa yana leongo la kuvunja amani.

Kamishna Kova amesema Jeshi la Polisi watatumia uwezo wao kwa misingi ya sheria ili kudhibiti maandamano hayo ambayo hayana nia nzuri. 

“Maandamano yao hayana mantiki yoyote, tuliwaita viongozi wao ambao ni Maulid Said Naibu Katibu na Masoud Said Masoud ili waongozane na Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalumu  kwenda NEC kupata ufumbuzi wa maoni yao,” alisema Kova.

Posted by MROKI On Thursday, February 12, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo