Nafasi Ya Matangazo

February 07, 2015

Mabingwa wa kombe la Mapinduzi, Simba ya Dar es Salaam leo imegawana pointi na Mbwa Mwitu wa Tanga, Coast Union katika mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara uliopigwa jioni ya leo katika uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga na kutoka sare ya bila ya kufungana.

Wanyama hao wa mwituni wamemaliza dakika 90 za kusukuma gozi la Ngombe bila goli hata la kuotea. Coast Union  siku kadhaa zilizopita iliambulia kichapo cha goli moja kutoka kwa Yanga ya daes salaam.

Kikosi cha Simba SC kiliwakilishwa dimbani na: Ivo Mapunda, Kessy Ramadhani, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Hassan Isihaka, Juuko Murshid, Jonas Mkude, Simon Sserunkuma/Messi dk79, Abdi Banda, Dan Sserunkuma/Ibrahim Hajibu dk88, Elias Maguri na Emmanuel Okwi.

Kikosi cha Coastal Union wao ilikuwa: Shaaban Kado, Mbwana Hamisi, Othman Tamim, Abdallah Mfuko/Hamad Juma dk59, Juma Lui, Abdulhalim Humud, Joseph Mahundi/Itubu Imbem dk86, Godfrey Wambura, Bright Ike Obinna/Mohammed Mtindi dk66, Hussein Sued na Rama Salim.
Posted by MROKI On Saturday, February 07, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo