Miss
Singida na Miss Kanda ya Kati 2014/15 ,Doris Mollel akisikiliza jambo kutoka
kwa Afisa Mipango wa Children’s Book Project for Tanzania,Ramadhani Ali
wakati akipokea vitabu kutoka Children’s Book Project for Tanzania.
*********
SHULE tatu za msingi katika mkoa wa Singida,zitapokea vitabu 200 wiki hii
kusaidia katika mchakato wa kuboresha elimu ya shule ya msingi. Vitabu
hivi vimetolewa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Children’s Book
Project for Tanzania na italenga maelfu ya watoto nchini kote katika
kuwakomboa kielimu.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi vitabu hivyo,Afisa Mipango wa Children’s Book
Project for Tanzania,Ramadhani Ali alisema kuwa Watoto wanaotakiwa
kupata vitabu hivi ni wale walio na uhitaji sana na watapata nafasi ya
kunufaika zaidi kielimu.
"Watoto
wanaopata vitabu hivi ni wale walio na uhitaji sana na watapata nafasi
ya kunufaika zaidi kielimu. vitabu hivi vinatolewa kwa watoto ili waweze
kutumia katika masoma yao ya kila siku shuleni.” alisema Ramadhani
Msaada
huu wa vitabu umejikita katika kukomboa hali ya elimu Tanzania, huku
serikali ikijitahidi kuwekaza katika elimu nchini kwa kipindi kirefu.
Inakadiriwa kuwa asilimia kubwa ya watoto wa shule ya msingi Tanzania
hawajui kusoma na kuandika,Ukosefu wa vitabu unachangia wanafunzi wa
shule ya msingi kushindwa kusoma na kuandika.
Tafiti
mbalimbali kutoka za serikali na sekta binafsi zinaonyesha wazi kuwa
kujifunza kusoma mapema ni uwekezaji katika siku zijazo kwa mtoto,kwani
elimu katika ngazi ya chini kwa mwanafunzi inachangia kuboresha maisha
yake ya baadae.
Kwa
upande wake Doris Mollel ambaye ni Balozi wa Elimu mkoani Singida
anatambua umuhimu wa elimu katika ngazi ya chini na anatumia muda wake
mwingi katika harakati za kukomboa elimu ya shule ya msingi. Ziara zake
nyingi hujikita katika mikoa ya ukanda wa kati hususani Singida na
Tanzania kwa ujumla,Vile vile ni mshauri wa wanafunzi wa shule za
msingi.
"Msingi
wa kujifunza kusoma hufungua uwezo wa kufikiri kwa mwanafunzi akiwa na
umri mdogo bila kiini hiki cha msingi maendeleo na mafanikio ya
mwanafunzi ni magumu.” alisema Doris
Doris
Mollel ni Miss Singida kanda ya kati 2014/15 na analenga katika
kuboresha maisha ya jamii kwa kupitia elimu na masuala mengine ya
kitamaduni.
endelevu
ReplyDelete