Kutoka kushoto ni Ofisa habari wa Red Arrows Lt Melody Siisii,
Mwenyekiti wa Red Arrows Col Nolasco Chilando, Katibu Mkuu wa TFF
Selestine Mwesigwa na Ofisa Ubalozi wa Zambia nchini Tanzania Alex
Chila, wakiwa ofisi za TFF - PPF Tower leo.
*********
Klabu ya Red Arrow FC
inayoshiriki Ligi Kuu nchini Zambia inatarajiwa kuwasili jijini Dar es
salaam-Tanzania jumatatu ya wiki ijayo kwa ajili ya kuweka kambi ya mafunzo ya
wiki moja kujindaa na msimu mpya wa Ligi Kuu nchini humo 2015.
Uongozi wa klabu hiyo
chini ya mwenyekiti wake Col Nolacso K Chilando ulifika leo makao makuu ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania - TFF sambamba na Afisa habari wa
klabu Lt Col Melody Siisii, Bw Alex Chila ofisa ubalozi wa Zambia nchini
Tanzania kujitambulisha uwepo wao nchini.
Wakiongea na
katibu mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania - TFF
Selestine Mweisgwa, uongozi wa timu hiyo umesema maandalizi ya kambi
yameshakamilika na kikubwa walikua wanaliomba Shirikisho la Mpira wa Miguu
nchini kutambua uwepo wao na kuwasaidia kupata viwanja vya kufanyia mazoezi.
Naye Katibu Mkuu wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini -TFF Bw.Mwesigwa alisema wameyapokea
maombi hayo ya Red Arrow FC na kuwakaribisha nchini kwa ajili ya kambi
yao na kusema ujio wao utafungua milango kwa vilabu vingine pia kuja kuweka
kambi nchini.
Timu ya Red Arrow FC
inayomilikiwa na jeshi la Anga nchini Zambia ikiwa nchini kwa mafunzo, inatarajia
kucheza mchezo mmoja wa kirafiki na imeliomba Shirikisho la Mpira wa Miguu
nchini kuwatafutia timu moja ya kucheza nayo.
0 comments:
Post a Comment