Mwenyekiti
wa Kamati ya Maandalizi ya Sherehe za Maadhimisho ya miaka 38 ya CCM,
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Songea, Dk. Emmanuel Nchimbi
akizungumza katika maadhimisho ya miaka 38 ya CCM, yaliyofanyika kitaifa
juzi kwenye Uwanja wa Maji Maji mjini Songea,
Mkoani Ruvuma.Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete,
Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Maandalizi ya Sherehe za Maadhimisho ya miaka 38 ya CCM,
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Songea, Dk. Emmanuel Nchimbi (kulia)
akijadiliana jambo na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula
(katikati) pamoja na Katibu Mkuu wa chama hicho,
Abdulrahman Kinana.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Maandalizi ya Sherehe za Maadhimisho ya miaka 38 ya CCM,
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Songea, Dk. Emmanuel Nchimbi
akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Bernard Membe katika maadhimisho ya miaka 38 ya
CCM, yaliyofanyika kitaifa juzi kwenye Uwanja wa Maji Maji mjini
Songea, Mkoani Ruvuma katikati ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Ruvuma Oddo
Mwisho.
*********
Na Mwandishi Wetu
Mwenyekiti
wa maandalizi ya sherehe za maika 38 ya Chama Chama Cha Mapinduzi (CCM)
ambaye pia ni mbunge wa Songea mjini Dkt Emmanuel Nchimbi amesema
kuwa chama chake kina kila sababu ya kushinda kwa kishindo kwenye
uchaguzi mkuu wa mwaka huu kwa kuwa kina mfumo na muundo imara.
Akizungumza
muda mfupi baada ya maadhimisho hayo mjini Songea, Dkt Nchimbi ambaye
pia ni mjumbe wa halmashauri kuu ya chama hicho alisema kuwa chama
chake hakina tatizo la kimfumo wa muundo na kuongeza kuwa ushindi ni
lazima.
“Chama
hakina tatizo la muundo wala mfumo na tutakachofanya ni kubadilisha
mikakati tu ili kujihakikishia ushindi katika uchaguzi ujao,” alisema
Aliongeza,
“Kwa kwa kaida hakuna mkakati unadumu. Mar a zote mikakati hubadilika
kulingana na mazingira na hiki ndicho tutakachokifanya,”
Akizungumzia
kuhusu kauli ya mwenyekiti wa chama hicho Rais Jakaya Kikwete kuwataka
viongozi wa chama kuwatembelea wanachama na kushawishi wanachama
wapya, alisema CCM ni chama kikubwa na ndani yake wapo viongozi
waliolala ambao mwenyekiti wa taifa aliwakumbusha kuamka na kufanya
kazi.
“Chama
hakiwezi kuwa na maisha marefu kama viongozi katika ngazi zote ha
hawajitumi. Katika jeshi kubwa kama hili la CCM wapo watu ambao lazima
wasukumwe
na ndiyo ahwa mwenyekiti wetu wataifa aliwasukuma kupitia hotuba yake.
Hawa
wanatakiwa kuamka na kuanza kufanya kazi kwa bidii ili kukiwezesha
chama kushinda kwa kishindo kama ambavyo kimekuwa kikishinda tangu
kuanza
kwa siasa za vyama vingi,” alieleza
Dkt
Nchimbi aliishukuru halmashauri kuu ya chama kwa kuweza kuuchagua mkoa
wa Ruvuma kwa ajili ya maazimisho ya miaka 38 ya chama hicho na kueleza
kuwa kwa miaka mingi Ruvuma imekuwa ngome imara ya CCM.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa CCM mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho alisema kuwa
alisema kuwa chama chake kimeshaanza kujipanga kwa ajili ya uchaguzi
mkuu
.
“Nimeshawaagiza
viongozi wa chama katika ngazi ya mkoa na wilaya kuanza vikao kwa ajili
ya na kuweka mikakati thabiti ya ushindi katika uchaguzi mkuu
ujao,”
Alieeleza
kuwa, chama katika mkoa wake tayari kilishaanza mikakati ya
kujitegemeza ikiwa ni kufuata agizo la mwenyekiti wa taifa ambapo tayari
kimejipanga
vyema kuendeleza vyanzo vyake vya mapato pamoja na kuanzisha vyanzo
vipya kwa ajili ya kukifanya kujitegemea
0 comments:
Post a Comment