Tarehe 24/02/2015
katika Mahakama ya Wilaya ya Mpwapwa Mkoa wa Dodoma, mtu mmoja anayefahamika
kwa jina la YUSUPH CHATAMBALA, umri miaka 45, kabila Mchaga, Mkulima na mkazi
wa Kijiji cha MAKUTUPA Kata ya Lupeta Wilayani Mpwapwa Mkoa wa Dodoma,
amehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la KUNAJISI mtoto wa miaka mine (4).
Mwendesha Mashitaka
wa Polisi katika Mahakama ya Wilaya ya Mpwapwa Mkaguzi Msaidizi wa Polisi GODWILL S. IKEMA (A/Insp) akisoma mashitaka
Mahakamani alisema, Mtuhumiwa alitenda kosa la KUBAKA lililo kinyume cha sheria
za nchi chini ya Kifungu namba 130 (1) 2 (a) na 131 (1) cha Kanuni ya Adhabu kama
kilivyofanyiwa mapitio mwaka 2002.
YUSUPH CHATAMBALA alitenda kosa hilo siku ya
tarehe 20/02/2015 saa 12:00 jioni, huko kijiji cha Makutupa Wilaya ya Mpwapwa
Mkoa wa Dodoma, ambapo alimbaka mtoto mdogo wa kike mwenye miaka 04 (jina
limehifadhiwa). Alitenda kosa hilo baada ya kumkamata alipokuwa akicheza na
watoto wenzake jirani na nyumbani kwao kisha kumpeleka kwenye shamba la mahindi
kisha KUMNAJISI mtoto huyo na kusababishia majeraha na maumivu makali.
Mtuhumiwa
alifikishwa mahakamani siku ya tarehe 23/02/2015 na kusomewa shitaka lake,
ambapo alikiri kutenda kosa hilo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya
ya Wilaya ya Mpwapwa Mh. PASCHAL F. MAYUMBA. Siku ya tarehe 24/02/2015
alifikishwa tena Mahakamani hapo na kusomewa tena shitaka lake na kukiri tena
kutenda kosa hilo.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpwapwa Mh.
PASCHAL F. MAYUMBA alimtia hatiani
mtuhumiwa huyo baada ya kukiri kutenda kosa hilo. Akisoma hukumu hiyo; Mh.
Hakimu Mkazi Mfawidhi, alisema Mahakama inamhukumu
kwenda Jela Kifungo cha Maisha kwa
kosa la Kumnajisi mtoto ili kuwa
fundisho kwake na kwa wengine wanaotenda makosa kama hayo.
Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi D. A. MISIME – SACP alithibitisha
kuwepo kwa tukio hilo na hukumu iliyotolewa dhidi ya mtuhumiwa huyo. Kamanda
Misime alisema Makosa ya Unyanyasaji wa Kijinsia yamekuwa yakichukuliwa hatua
kali kutokana na uelewa wa wananchi juu ya ubaya wa vitendo vinavyofanywa na
kutolea taarifa bila woga katika Madawati yanayoshughulikia kesi hizo katika
vituo vya Polisi. Alisisitiza kuwa wananchi waendelee kushirikiana na Jeshi la
Polisi kuwafichue wahalifu wa makosa yote na kuyafanya makazi yao kuwa sehemu
salama ya kuishi na kujiletea maendeleo bila hofu dhidi ya wahalifu.
Imetolewa na Idara ya Habari na Matukio Polisi Mkoa wa
Dodoma.
KNY: Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma
Picha iliyotumika ni ya Gereza Kuu la Kigali Nchini Rwanda
Picha iliyotumika ni ya Gereza Kuu la Kigali Nchini Rwanda
0 comments:
Post a Comment