Nafasi Ya Matangazo

February 02, 2015

 Mwanamasumbwi maarufu Francis Cheka akiwa chini ya ulinzi wa Polisi baada ya kuhukumu ya miaka 3 jela.
 Akikwea gari la polisi
BONDIA nyota wa ngumi za kulipwa nchini aliyewahi kuwa Bingwa wa Dunia wa WBF, Francis Cheka 'SMG' mwenye maskani yake mjini Morogoro amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela.
Kwa mujibu wa kituo cha redio cha EFM kipindi cha Sports Headquarter, Cheka amehukumiwa adhabu hiyo baada ya kukutwa na hatia ya kumpiga mtu aliyekuwa mbia wake katika biashara ya ukumbi wa DDC-Morogoro aliyekuwa akidaiana naye.
Akizungumza na kituo hicho baba mzazi wa Francis Cheka amesema haikuwa sahihi kwa mwanae kupewa hukumu hiyo na badala yake wangekaa na kuzungumza ili kuyamaliza matatizo hayo.
Mzee huyo alienda mbali zaidi na kusema kuwa kuna watu wenye chuki na mwanae wameitumia kesi hiyo ya muda mrefu kutimiza malengo yao lakini pia mzee huyo ameelezea hisia zake kwa wakazi wa Morogoro kutoa sapoti ndogo kwa mwanae.
Taarifa zinasema kuwa Cheka amehukumiwa adhabu hiyo leo JUmatatu Februari 2, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro.source:MZUKA WA FUNGO BLOG
Posted by MROKI On Monday, February 02, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo