Nafasi Ya Matangazo

December 31, 2014


Watoto wanaolelewa katika kituo cha New Hope Family wakiwa wamebeba mzigo ya vyakula mbalimbali baada ya kukabidhiwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga( Tcaa) kwa ajili ya kusherehekea mwaka mpya.
Afisa habari wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Ali Changwila akimkabidhi Diana Amri msaada wa madaftari ya shule kwaniaba ya wenzake wakati walipokwenda kutoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo vyakula kwa kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha kuleta yatima cha New Hope Family chenye watoto 36. Kilichopo mwasonga kigamboni jijini kata ya kisarawe 2. Temeke jijini Dar es Salaam.
Afisa habari wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Ali Changwila akimkabidhi Peter Benard gunia la mchele kwaniaba ya wenzake wakati walipokwenda kutoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo mafuta ya kupikia na madaftari kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha kuleta yatima cha New Hope Family chenye watoto 36. Kilichopo mwasonga kigamboni jijini kata ya kisarawe 2 ,Temeke jijini Dar es Salaam.
Mshauri wa Kituo cha kule watoto yatima wanaoishi katika mazingira magumu cha New Hope family Maiko Lugendo ,( kulia) akimuonyesha Afisa habari wa Mamka ya usafiri wa anga Tanzania (TCAA) Ali Changwila wakati walipokwenda kutoa msaada wa vitumbalimbali vikiwemo vyakula kwa ajili ya kusherehekea mwaka mpya kwenye kituo hicho kilichopo Mwasonga Kata ya Kisarawe 2 Kigamboni jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Hellen Erasto.
Afisa habari wa Mamlaka ya usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Ali changwila (katikati) akipewa maelezo na Mshauri wa Kituo cha kule watoto yatima wanaoishi katika mazingira magumu cha New Hope family Maiko Lugendo, wakati alipotembelea chumba cha kulala watoto wa kituo hicho wakati walipokwenda kutoa msaada wa vitumbalimbali vikiwemo vyakula kwa ajili ya kusherehekea mwaka mpya kwenye kituo hicho kilichopo Mwasonga Kata ya Kisarawe 2 Kigamboni jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Hellen Erasto.
Afisa habari wa Mamlaka ya usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Ali changwila akiwa amemnyenyua mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo cha New Hop e Family kilichopo Mwasonga kata ya Kisarawe 2 Kigamboni katika wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, wakati walipokwenda kutoa msaada wa vitumbalimbali vikiwemo vyakula kwa ajili ya kusherehekea mwaka mpya kwenye kituo hicho chenye watoto 36.
Baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo cha New Hope Family cha Mwasonga kilichopo Kigamboni ,Kilichoanzishwa 15 mwezi wa tisa 1999. Wakimsikiliza kwa makini afisa habari wa Mamlaka ya usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Ali changwila,(hayupo pichani) wakati aliokuwa akiongea nao baada ya kuwakabidhi msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo vyakula .
Posted by MROKI On Wednesday, December 31, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo