Na MatukiodaimaBlog
MBUNGE
wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati (CCM) amewakata
wananchi kutokubali kudanganywa na vyama vya siasa vinavyounda
umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) juu ya mchakato wa katiba
iliyopenekeshwa na badala yake kuungana na watanzania wapenda
maendeleo kuikubali katiba hiyo muda utakapofika.
Mbuge
Kabati alitoa kauli hiyo kwa nayakati tofauti juzi na jana
wakati wa semina zake za ndani na wanawake wanachama wa UWT
katika wilaya ya Iringa , Kilolo na Mufindi semina iliyolega
kuwajengea uwezo wa kujiamini kwa wanawake waliojitokeza kugombea
nafasi mbali mbali za uongozi wa serikali za mitaa na vijijini .
"
Mimi kama mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa wajibu wangu
ni pamoja na kukutana na wananchi wa Iringa na kuwajengea uelewa
mpana wa katiba hiyo iliyopendekezwa ila muda ukifika wa
serikali kutangaza mchahato wa kupokea maoni ya wananchi juu ya
katiba hiyo iliyopendekezwa basi viongozi hao waweze kuelewa
zaidi pamoja na wananchi wanaowazunguka..... hivyo nitaendelea
kutoa elimu kwa viongozi wa chama katika semina mbali mbali"
Kabati
alisema kumekuwepo na upotoshwaji mkubwa ambao umeendelea
kufanywa na UKAWA kwa kuzunguka huku na kule kujaribu kupotosha
ukweli juu ya katiba iliyopendekezwa kwa madai kuwa ni katiba
ya CCM jambo ambalo ni upotoshaji mkubwa na kuwa mchakato wa
katiba hiyo ulifanywa na vyama vyote na makundi maalum.
Pia
alisema kuwa kitendo cha baadhi ya wanasiasa wasilolitakia
mema Taifa hili kwa kupotosha juu ya katiba hiyo ni sawa na
kutaka kuona nchi haitawaliki na hivyo kuamua kuanza
upotoshaji huo.
Alisema
kuwa si kweli kama katiba hiyo iliyopendekezwa haina jambo lolote
la msingi kama ambavyo UKAWA wamekuwa wakizunguka na kupotosha
ila alidai kuwa ndani ya katiba hiyo kuna mambo mengi
yamezingatiwa kwa ajili ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
Akielezea
kuhusu mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa ,vijiji na
vitongoji unaotaraji kufanyika hivi karibuni alisema kuwa upande
wa mkoa wa Iringa wanawake baada ya kuhamasishwa wamepatika
kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu za kuwania nafasi mbali mbali
za uongozi na kuwa baadhi ya maeneo wamepata kushinda kwa kishindo
nafasi walivyoomba ndani ya CCM wakisubiri uchaguzi rasmi wa
serikali .
Hivyo
aliwataka wananchi wa mkoa wa Iringa kujitokeza kuwapa kura zao
wanawake hao waliogombea nafasi mbali mbali na kuwa imani yake
kuona kunakuwa na uongozi mchanganyiko.
|
0 comments:
Post a Comment