Meneja
Masoko na Mauzo wa Azma Media, Mgope Kiwanga (kushoto),Ofisa Masoko na Mauzo, Shah Mrisho (kati) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Limited, Rhys Torringotn wakiwa katika mkutano na wanahabari Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa Promosheni ya 'Mtonyo
Chapchap' ya Azam TV, iliyoanza leo na itaendelea hadi Desemba 31,
mwaka huu.
Mtendaji
Mkuu wa Azam Media Limited, Rhys Torringotn (kulia) akizungumza na
waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam makao makuu ya kampuni hiyo, TAZARA,kuhusu promosheni ya hiyo ya 'Mtonyo
Chapchap' ya Azam TV, ambayo imeanza leo na itaendelea hadi Desemba 31,
mwaka huu. Pamoja nae ni Meneja
Masoko na Mauzo, Mgope Kiwanga.
Azam Media Limited leo wamezindua rasmi promosheni ya 'Mtonyo chapchap' ambayo ni moja ya shamra shamra zake za kutimiza mwaka tangu kuanzishwa kwa kampuni hiyo.
Mtonyo Chapchap itadumu hadi Desemba 31 mwaka huu na itampatia mteja gharama ya fedha aliyotumia kununua kisumbusi ambayo ni shilingi 165,00/= .
Mteja anaetaka kuingia katika droo hiyo, anatakiwa kununua kisumbusi kipya vya Azam TV na kukiwekea malipo ya mwezi na promosheni hiyo itawahusu wateja wapya na wazamani.
Kutakuwa
na washindi 100 watakaopatikana katika kipindi chote cha
kampeni hiyo ambao watakuwa wakitangazwa kila wiki kupitia kwenye vyombo
habari, mbalimbali kama vituo vya Radio, Televisheni, Magazeti na magazeti tando (blogu).
Wiki ya kwanza, watangazwa washindi 15, kama ambavyo itakuwa
katika wiki ya pili, wakati ya tatu watatangazwa washindi 20 kabla ya
wiki ya mwisho kutangazwa washindi 50.
0 comments:
Post a Comment