Nafasi Ya Matangazo

November 03, 2014

 Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimvisha mwanafunzi mlemavu wa kusikia (kiziwi) Bertha Samwel wa darasa la tatu Shule ya msingi Buguruni, Kifaa maalum cha kumwezesha kusikia, wakati wa uzinduzi rasmi utoaji wa huduma kwa walemavu wa kusikia (Viziwi). Uzinduzi huo umefanyika leo Novemba 3, 2014 kwenye Viwanja vya Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, chini ya usimamizi wa Taasisi ya Starkey Hearing ya nchini Marekani.
 Makamu wa Rais wa Jasmhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Mwasisi wa Taasisi ya Starkey Hearing, William Austine, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi walemavu wa kusikia, wakiopatia mashine maalum za kuwawezesha kusikia, baada ya kuvishwa mashine hizo wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo.
 Mwanafunzi Amina, akivishwa kifaa hicho...
 Makamu wa Rais Dkt. Bilal, akiwasili katika hafla hiyo...
 Baadhi ya wanafunzi wenye ulemavu wa kusikia, (Viziwi) wakisubiri kupatiwa huduma hiyo wakati wa uzinduzi.
 Baadhi ya wanafunzi wenye ulemavu wa kusikia, (Viziwi) wakisubiri kupatiwa huduma hiyo wakati wa uzinduzi.
Posted by MROKI On Monday, November 03, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo