Nafasi Ya Matangazo

November 07, 2014

 Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote (Dangote Group of Industries), Alhaji Aliko Dangote akiwa kwenye gari huku akipata maelezo ya ujenzi wa kiwanda hicho kutoka kwa mafundi na wahandisi ya Dil & Sinoma inayojenga kiwanda hicho kitakachokuwa cha tatu kwa ukubwa Afrika.
 Msafara wa Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote (Dangote Groupof Industries), Alhaji Aliko Dangote, ukikagua ujenzi wa kiwanda hicho kinachotarajiwakuanza kazi Aprili, mwakani. Awamu ya kwanza ya kiwanda hicho ujenzi wake ukikamilikakitakuwa kinazalisha tani 6000 kwa siku. 
 Dangote akiangalia moja ya majengo yanayoendelea kujengwa kiwandani hapo
 Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote (Dangote Group of Industries), Alhaji Aliko Dangote (kulia) mfanyabiashara maarufu kutoka Nigeria, akizungumza na Meneja Mkuu wa Kiwanda kikubwa cha cha saruji cha Dangote Tanzania, Daljit Singh (katikati), alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho,mkoani Mtwara. Kushoto ni Kenneth Kasigila ambaye ni Msaidizi Maalumu wa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, iliyopewa fursa ya kwanza kujenga benki karibu na kiwanda hicho.

 Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba, ambaye ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Ponsiano Nyami (kushoto), akizungumza na Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote (Dangote Group of Industries), Alhaji Aliko Dangote, muda mfupi kabla ya mfanyabiashara huyo kuondoka Uwanja wa Ndege wa Mtwara jana, baada ya kukagua ujenzi wa kiwanda chake.
 Dangote akisindikizwa kwenda kupanda ndege kwenye Uwanja wa Ndege wa Mtwara
 Dongote akiagana na Kaimu Mkuu wa Mkoawa Mtwara, Ponsiano Nyami
 Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote (Dangote Group of Industries), Alhaji Aliko Dangote, akiaga alipokuwa akiondoka na ndege yake kwenye Uwanja wa Ndege wa Mtwara jana. Alitumia takribani saa mbili kuwepo nchini, baada ya kuwasili asubuhi saa 1:42 na kuondoka saa 3:42 baada ya kupata maelezo ya ujenzi na kukagua kiwanda chake.
 Ndege ikiwa imepaa
Posted by MROKI On Friday, November 07, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo