Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar
Pistorius amehukumiwa jela miaka 5 baada ya kupatikana na hatia ya
kumuua mpenziwe Reeva Steenkamp.
Hii ni baada ya mwanariadha huyo mlemavu kupatikana na hatia ya mauaji bila ya kukusudia.
Jaji
aliyetoa hukumu hiyo,Thokozile Masipa,alianza kutoa kauli yake ya
mwisho kabla ya kutoa hukumu saa mbili na nusu asubuhi na akasema ni
changamoto kubwa kwake kupata adhabu ambayo itaridhisha pande zote
kwenye kesi hiyo.
Upande wa mashitaka ulitaka mwanariadha huyo
kupewa kifungo cha miaka 10 gerezani baada ya kupatikana na makosa ya
kuua bila kukusudia.
Pistorius alisema kuwa alifyatua risasi baada ya kudhani kuwa jambazi alikuwa amevamia nyumba yake.
Upande
wa mashitaka ulisisitiza Pistorius afungwe jela wakati wakili wa
Pistorius wakimtaka jaji ampe kifungo cha nyumbani cha miaka mitatu na
pia apewe usaidizi na ushauri wa kubadili tabia yake.
Jaji alisema
kuwa Pistorius asingepewa adhabu ya kifungo cha nyumbani kwani hukumu
kama hiyo ingekuwa hatua mbaya na mfano mbaya kwa wahalifu.
0 comments:
Post a Comment