Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa
Elisante Ole Gabriel akizungumza katika uzinduzi wa mbio za Uhuru
Marathon Dar es Salaam jana.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akizungumza katika uzinduzi wa mbio za Uhuru Marathon Dar es Salaam jana. Kulia ni Mratibu wa Mbio hizo kutoka Kampuni ya Intelectual Communication, Innocent Meleck.
*********
MASHINDANO ya mbio nefu za Uhuru Marathon ambayo yamepangwa kufanyika
Desemba 7 mwaka huu yamezinduliwa rasmi jana jijini Dar es Salaam kwa kuwataka
wanariadha kujitokeza ili kuimarisha Amani,afya, uhuru, uzalendo na muungano wa
Watanzania.
Akizungumza jana jijini, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo, Prof Olisante Ole Gabriel , alisema kuwa anaipongeza Kamati ya
Maandalizi ya mbio hizo kwa sababu zinalengo la kihistoria la kumbukumbu za
Uhuru wa Tanzania.
Prof
Elisante aliwaomba wahisani mbalimbali kujitokeza kwa wingi na
kudhamini mbio hizo huku akisisitiza kuwa serikali ipo bega kwa bega
katika kuhakikisha ujumbe wa mwaka huu unawafikia walengwa ambao ni
jamii nzima ya kitanzania na wapenda amani wote ulimwenguni
Ndugu
zangu serikali inawaomba kwa dhati kabisa watu na mashirika mbalimbali
ya kiserikali na mashirika binafsi kujitokeza kwa wingi katika kudhamini
mbio hizi kwa kuwa lengo lake ni chanya kwa taifa letu,hata pale
serikali itakapohitajika kutoa ushirikiano wowote basi kama serikali
tupo tayari kwa hilo muda wowote ,
Alisema kuwa kupitia mbio hizo suala la Amani litasisitiza na
hakuna mahali popote duniani ambapo wananchi wake hawapendi Amani.
“Mbio hizi zinafanyika huku jambo muhimu likiwa ni kusisitiza na
kuuenzi Muungano wetu katika jamii iliyostahamilivu,” alisema kiongozi huyo wa
wizara.
Aliwataka pia wenyeji wa mbio hizo, Chama cha Riadha mkoa wa Dar
es Salaam (DAAA) kusimamia kikamilifu mbio hizo kwa sababu ni sehemu ya
kuwaandaa wanariadha na mashindano mengine ya kimataifa watakayoshiriki.
Mratibu wa mbio hizo, Innocent Melleck, alisema kuwa mbali na
kuendeleza vipaji vya wanariadha, mbio za Uhuru Marathon zina lengo la
kuhamasisha Amani, umoja na mshikamano wa wananchi wa Tanzania.
Melleck alisema kuwa kupitia mbio hizo pia wananchi watashiriki
kusisitiza Muungano uliopo hapa nchini.
Alisema kuwa anaamini mbio za mwaka huu zitasaidia kuutangaza
mchezo wa riadha ambao miaka ya nyuma uliipa sifa kubwa Tanzania kwa wanariadha
wake kupata medali katika mashindano ya kimataifa.
Aliongeza kuwa katika mbio hizo, wanariadha watachuana katika
marathoni, nusu marathoni na mbio maalumu za kujifirahisha za kilomita tano.
Melleck aliitaja kauli mbiu ya mbio za mwaka huu ambazo zitaanzia
kwenye viwanja vya Leaders jijini ni “ Uhuru Wetu, Amani Yetu, Tuitunze”
Naye Katibu Msaidizi wa DAAA, Ombeni Zavalla, alisema kuwa chama
hicho kiko tayari kushirikiana na Kamati ya Maandalizi ili kufanikisha mbio
hizo zinafanyika kwa kufuata taratibu zote za kiufundi.
Mbio
za uhurumarathon zinafanyika kwa mwaka wa pili mfululizo hapa nchini
ambapo mwaka jana zilifanyika tarehe 08/12/2013 hapa jijini Dar Es
Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano
wa Tanzania Dr Mohamed Gharib Bilal ambapo jumla ya wanariadha 2618
walishiriki mbio hizo toka katika mataifa 21
0 comments:
Post a Comment