Mkurugenzi
wa Lino International Agency ambao ni Waandaaji wa mashindano ya Miss Tanzania,Hashim Lundenga (wapili kushoto) akifafanua kwa waandishi wa habari juu ya sakata la umri Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Mtemvu (kushoto),katika mkutano huo Lundenga
alitolea ufafanuzi swala la umri wa Mrembo huyo kulingana na vilelezo
alivyopewa na mrembo huyo wakati akijiunga na mashindano hayo. Wengine pichani ni Miss Tanzania namba mbili, Lilian Kamazima na Katibu Mkuu wa Kamati ya Miss Tanzania, Bosco Majaliwa.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiCACmYnd3T3nqdNS83-1yZIBUCDoZDVGMG34bRmJUXPvZZ2dJmo5djgSPytdMheZCAN0YM0UNmHF7jToj077YzNkas5ovabRV83OYeDJTxg2WgIvlzNn5eRFiXS3rT6G3d_lrlKeWSJ6ho/s1600/Sitti1.jpg)
Katika suala la kumvua taji hilo ama laa, Sitti Mtemvu, Lundenga amesema kamati yake haina mamlaka hayo bali ni Baraza la Sanaa la Taifa na Wizara husika ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Lundenga aliendelea kusema kuwa Mashindano ya Miss Tanzania hayaruhusu mshiriki yeyote mwenye mtoto kushiri,hivyo katika swala la Sitti Mtemvu kuwa ana mtoto,hilo kalina ukweli wowote bali ni uvumi tu wa kwenye mitandao ya kijamii baada ya Mrembo huyo kuonekana akiwa katika picha na mtoto alieomba kupiga nae.
0 comments:
Post a Comment